Shaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab (Rahimahu Allaah) amesema:

Ummah huu umefaradhishiwa kufanya Hijrah kutoka katika mji wa kikafiri na kwenda katika mji wa Kiislamu na itabaki mpaka Qiyaamah kitaposimama. Dalili ni maneno Yake (Ta´ala):

إِنَّ الَّذِينَ تَوَفَّاهُمُ الْمَلَائِكَةُ ظَالِمِي أَنفُسِهِمْ قَالُوا فِيمَ كُنتُمْ ۖ قَالُوا كُنَّا مُسْتَضْعَفِينَ فِي الْأَرْضِ ۚقَالُوا أَلَمْ تَكُنْ أَرْضُ اللَّـهِ وَاسِعَةً فَتُهَاجِرُوا فِيهَا ۚ فَأُولَـٰئِكَ مَأْوَاهُمْ جَهَنَّمُ ۖ وَسَاءَتْ مَصِيرًا إِلَّا الْمُسْتَضْعَفِينَ مِنَ الرِّجَالِ وَالنِّسَاءِ وَالْوِلْدَانِ لَا يَسْتَطِيعُونَ حِيلَةً وَلَا يَهْتَدُونَ سَبِيلًا فَأُولَـٰئِكَ عَسَى اللَّـهُ أَن يَعْفُوَ عَنْهُمْ ۚ وَكَانَ اللَّـهُ عَفُوًّا غَفُورًا

“Hakika wale ambao Malaika wamewafisha, hali ya kuwa wamejidhulumu nafsi zao, wataambiwa: “Mlikuwa katika hali gani?” Watasema: “Tulikuwa tukikandamizwa katika ardhi.”  Malaika watasema: “Je, kwani ardhi ya Allaah haikuwa pana mkahajiri ndani yake?” Basi hao makazi yao yatakuwa ni Moto – na ubaya ulioje mahali pa kurejea! Isipokuwa wale waliokandamizwa kati ya wanaume na wanawake na watoto ambao hawakuweza kupata namna yoyote wala hawawezi kuongoza njia. Basi hao huenda Allaah akawasamehe – na Allaah ni Mwingi wa kusamehe, Mwingi wa kughufiria.”[1]

Dalili ni Kauli Yake (Ta´ala):

يَا عِبَادِيَ الَّذِينَ آمَنُوا إِنَّ أَرْضِي وَاسِعَةٌ فَإِيَّايَ فَاعْبُدُونِ

“Enyi waja Wangu ambao mmeamini! Hakika ardhi Yangu ni pana, basi Mimi pekee niabuduni.”[2]

al-Baghawiy (Rahimahu Allaah) amesema:

“Sababu ya kuteremka Aayah hii kwa baadhi ya waislamu Makkah ambao hawakufanya Hijrah. Hivyo Allaah amewazungumzisha kwa jina la imani.”

MAELEZO

Maneno Yake (Ta´ala):

إِنَّ الَّذِينَ تَوَفَّاهُمُ الْمَلَائِكَةُ ظَالِمِي أَنفُسِهِمْ

“Hakika wale ambao Malaika wamewafisha, hali ya kuwa wamejidhulumu nafsi zao… “

Bi maana wamewafisha hali ya kuwa bado wanakaa kati ya makafiri. Hili ni jambo la khatari ambalo Allaah ametishia juu yake Moto. Allaah (´Azza wa Jll) amewabagua wale wanyonge na walioshindwa kufanya Hijrah.

Maneno Yake (Ta´ala):

يَا عِبَادِيَ الَّذِينَ آمَنُوا إِنَّ أَرْضِي وَاسِعَةٌ فَإِيَّايَ فَاعْبُدُونِ

“Enyi waja Wangu ambao mmeamini! Hakika ardhi Yangu ni pana, basi Mimi pekee niabuduni.”

Mtu anatakiwa kuhama kutoka katika maeneo ambayo hawezi kumwabudu Allaah na kwenda kwengine.

[1] 04:97-99

[2] 29:59

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Thalaathat-il-Usuwl, uk. 100
  • Imechapishwa: 16/02/2023