Shaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab (Rahimahu Allaah) amesema:

na akafaradhishiwa swalah tano kwa siku. Aliswali Makkah kwa miaka mitatu. Baada yake akaamrishwa kufanya Hijrah kwenda Madiynah. Hijrah ni kutoka katika mji wa kikafiri na kwenda katika mji wa Kiislamu.

MAELEZO

Allaah alimfaradhishia swalah khamsini. Alipofika katika mbingu ya sita Muusa (´alayhis-Salaam) akamuuliza ni swalah ngapi Mola wake amemfaradhishia ambapo akajibu kuwa ni khamsini. Akamwambia arejea kwa Mola wake na amwombe awafanyie wepesi ummah wake. Kwa sababu ummah wake ni wanyonge na hawatokubali swalah khamsini kwa siku. Akamuomba ushauri Jibriyl ambapo akampa ushauri. Akarudi kwa al-Jabbaar (Subhaanah) akamuondoshea swalah kumi. Kuna upokezi mwingine unaosema kuwa alipunguziwe swalah tano tano. Akawa anaenda akirudi mara kadhaa mpaka Allaah akampunguzia zikawa swalah tano. Muusa akamwamrisha zipunguzwe hizo swalah tano lakini hata hivyo akakataa na kusema: “Mimi nimemuomba Mola wangu mpaka sasa naona haya.” Akaita Mwenye kuita kutoka mbinguni: “Mimi nimekwishapitisha faradhi Yangu na nimewapunguzia waja Wangu. Haibadilishwi kauli Kwangu; ni swalah tano kiidadi lakini ni swalah khamsini kithawabu katika mizani. Hili linafahamisha utukufu wa jambo la swalah. Kwa hivyo alifaradhishiwa swalah tano.

Mtunzi (Rahimahu Allaah) amesema:                                                                

”Aliswali Makkah kwa miaka mitatu.”

Aliswali Makkah na wakati huo hakukuwepo swalah ya mkusanyiko. Kuhusu adhaana na swalah ya mkusanyiko ilifaradhishwa Madiynah.

Mtunzi (Rahimahu Allaah) amesema:

”Hijrah ni kutoka katika mji wa kikafiri na kwenda katika mji wa Kiislamu.”

Hijrah ni kuhama kutoka mji wa kishirki na kwenda katika mji wa Kiislamu. Hili litakuwepo mpaka kisimame Qiyaamah. Kuhusu kufanya Hijrah kwa kutoka Makkah ni jambo limekwisha tokea wakati ulipofunguliwa mji wa Makkah na ukawa mji wa Kiislamu. Dalili juu ya ulazima wa kufanya Hijrah kutoka mji wa kishirki na kwenda katika mji wa Kiislamu ni maneno yake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Hakuna Hijrah baada ya Ufunguzi.”[1]

[1] al-Bukhaariy (2783) na Muslim (1864).

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Thalaathat-il-Usuwl, uk. 98-99
  • Imechapishwa: 16/02/2023