5- Uombezi ambao Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) anashirikiana na wengineo katika Malaika, Mitume, mawalii na waja wema na watoto waliokufa kabla ya kubaleghe. Ni uombezi juu ya watenda dhambi chini ya shirki ambao wataombewa ili wasiingie Motoni. Endapo wataingia basi wataombewa watoke ndani yake. Uombezi aina hii ndio ambao umepingwa na Khawaarij na Mu´tazilah na wakasema kwamba ambaye amestahiki kuingia Motoni basi ni lazima aingie na mwenye kuingia hatotoka.

Mtunzi amesema:

“Naamini.. “

Bi maana nasadikisha na naitakidi. Maneno yake:

“.. uombezi wa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam).”

Ambao ni maalum kwake. Pia anaamini uombezi anaoshirikiana na wengine. Kwa sababu haya ndio madhehebu ya Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah. Maneno yake:

“… na kwamba ndiye mwombezi wa kwanza… ”

Imepokelewa katika Hadiyth inayozungumzia juu ya kisimamo[1]. Maneno yake:

“… na ndiye wa kwanza atakayekubaliwa uombezi wake.”

Waombezi ni wengi. Lakini yeye (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ndiye mwombezi wa kwanza. Pia ndiye wa kwanza atayeitikiwa katika waombezi. Hapa kuna Radd kwa wale wanaosema kuwa Shaykh anapinga uombezi.

[1] Muslim (2278) kupitia kwa Abu Hurayrah (Radhiya Allaahu ´anh).

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh ´Aqiydat-il-Imaam Mujaddid Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab, uk. 77-88
  • Imechapishwa: 15/05/2021