Shaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab (Rahimahu Allaah) amesema:

Mji wake ni Makkah. Allaah Amemtuma ili kutahadharisha shirki na kulingania katika Tawhiyd. Dalili ni Kauli Yake (Ta´ala):

يَا أَيُّهَا الْمُدَّثِّرُ قُمْ فَأَنذِرْ وَرَبَّكَ فَكَبِّرْ وَثِيَابَكَ فَطَهِّرْ وَالرُّجْزَ فَاهْجُرْ وَلَا تَمْنُن تَسْتَكْثِرُ وَلِرَبِّكَ فَاصْبِرْ

”Ee uliyejigubika! Simama na uonye! Na Mola wako mtukuze! Na nguo zako zitwaharishe! Maambukizi yote ya kishirikina epukana nayo! Na wala usitoe kwa kwa kutaraji kukithirishiwa! Na kwa ajili ya Mola wako subiri!”

قُمْ فَأَنذِرْ

“Simama na uonye!”

maana yake ni kutahadharisha shirki na kulingania katika Tawhiyd.

وَرَبَّكَ فَكَبِّرْ

“Na Mola wako mtukuze!”

Maana yake amtukuze kwa Tawhiyd.

وَثِيَابَكَ فَطَهِّرْ

“Na nguo zako zitwaharishe!”

Maana yake twahirisha matendo yako kutokana na shirki.

وَالرُّجْزَ فَاهْجُرْ

“Maambukizi yote ya kishirikina epukana nayo!”

Ni masanamu. Kuyakata, ina maana ya kuyaepuka na kujitenga nayo na watu wake. Miaka kumi alilingania katika Tawhiyd. Baada ya miaka kumi alipandishwa mbinguni…

MAELEZO

Alilingania katika zile sifa nzuri ambazo Allaah alimuwajibishia na akikataza shirki na pia yale matendo maovu ambayo Allaah amemkataza na sifa zenye kusemwa vibaya. Dalili ya utume wake ni yale yaliyotajwa katika Suurah al-Muddaththir pale aliposema:

يَا أَيُّهَا الْمُدَّثِّرُ قُمْ فَأَنذِرْ وَرَبَّكَ فَكَبِّرْ وَثِيَابَكَ فَطَهِّرْ وَالرُّجْزَ فَاهْجُرْ وَلَا تَمْنُن تَسْتَكْثِرُ وَلِرَبِّكَ فَاصْبِرْ

”Ee uliyejigubika! Simama na uonye! Na Mola wako mtukuze! Na nguo zako zitwaharishe! Maambukizi yote ya kishirikina epukana nayo! Na wala usitoe kwa kwa kutaraji kukithirishiwa! Na kwa ajili ya Mola wako subiri!”

Hii ni amri anaamrishwa awatahadharishe watu kutokamana na shirki. Vilevile anaamrishwa amtukuze Mola wake kwa Tawhiyd. Sambamba na hayo anaamrishwa ayasafishe matendo yake kutokamana na shirki.

Wakati mwingine hutajwa nguo na kukakusudiwa matendo. Kuna maoni pia yanayosema kuwa nguo kutokana na najisi. Lakini muhimu zaidi ni kuyatakasa matendo kutokamana na shirki. Shari´ah ya kuzisafisha nguo kutokana na najisi ni jambo liliwekwa Madiynah na hili tukio limetokea Makkah.

Maneno Yake (Ta´ala):

وَالرُّجْزَ فَاهْجُرْ

“Maambukizi yote ya kishirikina epukana nayo!”

Bi maana masanamu. Kwa msemo mwingine yaepuke masanamu na wenye nayo. Aidha jitenge nayo mbali na wenye nayo.

Mtunzi (Rahimahu Allaah) amesema:

“Miaka kumi alilingania katika Tawhiyd…. ”

Bi maana aliendea Makkah kufanya ulinganizi huu miaka kumi na hakukuteremka kitu kingine katika mambo ya Shari´ah; si zakaah, swawm, hajj wala swalah. Kwa hiyo kitu muhimu ni Tawhiyd kwa sababu ndio msingi wa dini na msingi wa mila. Matendo hayasihi isipokuwa kwa Tawhiyd. Jengine ni kuwa Makkah walikuwa washirikina. Kipindi chote cha miaka kumi alipokuwa akiishi kati yao alikuwa akiwalingania katika Tawhiyd peke yake. Baada ya hapo kipindi hicho ndipo kukateremka faradhi ya swalah kwa ujumla.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Thalaathat-il-Usuwl, uk. 94-95
  • Imechapishwa: 14/02/2023