58. Mfungaji anatakiwa kujiepusha na kufanya ghushi

Mfungaji anatakiwa kujiepusha na ghushi katika miamala yote kuanzia biashara, ukodishaji, uundaji, uwekaji rehani, kupeana nasaha na mambo mengine ya mashauriano. Kwani hakika kufanya ghushi ni katika dhambi kubwa. Mtume  (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amejiweka mbali na yule mwenye kufanya hivo. Amesema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Yule mwenye kutufanyia ghushi hatokani na sisi.”

Katika tamko lingine imekuja:

“Mwenye kufanya ghushi hatokani nami.”

Ameipokea Muslim.

Ghushi ni hadaa, usaliti, kupoteza amana na kupoteza uaminifu kati ya watu. Kila chumo linalotokana na ghushi basi hilo ni chumo baya na la haramu. Halimzidishii mwenye nalo isipokuwa kuwa mbali zaidi na Allaah.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majaalis Shahr Ramadhwaan, uk. 71
  • Imechapishwa: 23/04/2021