Swali 31: Katika baadhi ya miji mchana unarefuka urefu usiokuwa wa kawaida ambapo wakati mwingine yanafika masaa ishirini. Je, waislamu katika miji hiyo wanatakikana kufunga mchana mzima?

Jibu: Ndio, wanatakikana kufunga mchana mzima. Allaah (Ta´ala) amesema:

فَالْآنَ بَاشِرُوهُنَّ وَابْتَغُوا مَا كَتَبَ اللَّـهُ لَكُمْ ۚ وَكُلُوا وَاشْرَبُوا حَتَّىٰ يَتَبَيَّنَ لَكُمُ الْخَيْطُ الْأَبْيَضُ مِنَ الْخَيْطِ الْأَسْوَدِ مِنَ الْفَجْرِۖ ثُمَّ أَتِمُّوا الصِّيَامَ إِلَى اللَّيْلِ

“Basi sasa changanyikeni nao [waingilieni] na tafuteni Aliyokuandikieni Allaah kwenu. Kuleni na kunyweni mpaka ubainike kwenu weupe wa alfajiri katika weusi wa usiku. Kisha timizeni swawm mpaka usiku.”[1]

Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Usiku ukija hapa [mashariki] na ukaondoka mchana hapa [magharibi] na likazama jua, basi amekwishafungua mfungaji.”[2]

[1] 02:187

[2] al-Bukhaariy (1954) na Muslim (2526).

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: 48 mas-alatu fiy Swiyaam, uk. 29-30
  • Imechapishwa: 23/04/2021