Swali 58: Baadhi ya watu wanawatukuza watu na kushabikia maoni yao. Unawanasihi nini watu hawa?

Jibu: Ni wajibu kufuata haki pamoja na yeyote yule atakayekuwa nayo[1], na si kuwafuata watu wanaopingana na haki. Imaam Ahmad (Rahimahu Allaah) amesema:

”Nashangazwa na watu wanaoitambua haki ya wapokezi na usahihi wake lakini wanaiacha na kwenda katika maoni ya Sufyaan. Allaah (Ta´ala) amesema:

فَلْيَحْذَرِ الَّذِينَ يُخَالِفُونَ عَنْ أَمْرِهِ أَن تُصِيبَهُمْ فِتْنَةٌ أَوْ يُصِيبَهُمْ عَذَابٌ أَلِيمٌ

“Basi watahadhari wale wanaokwenda kinyume amri yake; isije kuwapata fitina au ikawapata adhabu iumizayo.”[2]

Ibn ´Abbaas (Radhiya Allaahu ´anhumaa) amesema:

”Mawe yanakaribia kukushukieni kutoka mbinguni; nawaambie Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema na nyinyi mnasema Abu Bakr na ´Umar wamesema.”[3]

Ikiwa haya matahadharisho ni juu ya kuwafuata viumbe bora kabisa baada ya Mitume (Swalla Allaahu ´alayhim wa sallam) pasi na dalili, kusemwe nini juu ya kumfuata ambaye haitambuliki elimu wala ubora wake isipokuwa tu ni hodari wa kuongea?

[1] al-Awzaa´iy (Rahimahu Allaah) amesema:

”Tunazunguka na Sunnah kule inakoelekea.” (Sharh Usuwl I´tiqaad Ahl-is-Sunnah wal-Jamaa´ah (1/64))

[2] 24:63

[3] Ahmad (3121).

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Ajwibah al-Mufiydah ´an As-ilat-il-Manaahij al-Jadiydah, uk. 158-159
  • Imechapishwa: 24/03/2024
  • taaliki: Shaykh Jamaal bin Furahyaan al-Haarithiy