Abu Ja´far at-Twahaawiy (Rahimahu Allaah) amesema:

92 – Kuhiji na kupigana jihaad ni mambo yenye kuendelea na mtawala wa kiislamu, ni mamoja mwema na muovu wao, mpaka kisimame Qiyaamah. Hakuna kitu kitakachoyabatilisha wala kuyaondoa.

MAELEZO

Kuna jihaad aina mbili:

1 – Faradhi kwa watu wote. Ni kule kuwazuia maadui wanaoshambulia baadhi ya miji ya waislamu. Kama mfano wa mayahudi ambao wameivamia Palestina. Waislamu wote ni wenye kupata dhambi mpaka wawandoe humo.

2 – Faradhi kwa baadhi ya watu. Ikisimamiwa na baadhi basi haiwi wajibu kwa wengine. Hii ni jihaad kwa njia ya kufikisha ulingano wa Kiislamu kwenda katika miji mingine ili Uislamu utape kutawala. Ni vyema kwa wale watakaojisalimisha katika wakazi wake. Na ambaye atajaribu kuzuia basi atauliwa mpaka neno la Allaah liweze kushinda. Hii ya pili ni jihaad yenye kuendelea mpaka siku ya Qiyaamah, mbali na ile ya kwanza.

Miongoni mwa mambo yanayosikitisha ni kuwa wako baadhi ya waislamu hii leo wanaoipinga. Si hilo peke yake, bali wanafanya jambo hilo ni miongoni mwa sifa za kipekee za Uislamu. Hilo ni kutokana na sababu ya unyonge wao na kushindwa kwao kusimamia jihaad ambayo ni faradhi kwa watu wote. Amesema kweli Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) pale aliposema:

“Mtakapouziana kwa ribaa, mkashika mikia ya ng’ombe, mkaridhia kulima na mkaacha jihaad katika njia ya Allaah, basi Allaah atawasalitisha udhalili ambao hatauondoa mpaka mrudi katika dini yenu.”

  • Mhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-´Aqiydah at-Twahaawiyyah – Sharh wa Ta´liyq, uk. 83
  • Imechapishwa: 09/10/2024