Swali 57: Kama inavotambulika mswaliji akiwa mmoja basi anasimama kuliani mwa imamu. Je, imesuniwa kwake kusogea nyuma kidogo kama tunavoona baadhi wakifanya?

Jibu: Kilichowekwa katika Shari´ah kwa mswaliji akiwa peke yake asimame upande wa kuliani mwa imamu hali ya kulingana naye. Hakuna katika dalili za ki-Shari´ah yanayofahamisha kinyume chake.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa Muhimmah, uk. 60-61
  • Imechapishwa: 07/09/2022