Swali 56: Ni ipi hukumu ya uimamu wa ambaye anafanya baadhi ya madhambi kama uvutaji sigara, unyoaji ndevu, uburutaji nguo au mfano wake?

Jibu: Swalah yake ni sahihi akiswali kama ilivyowekwa na Allaah katika Shari´ah kwa maafikiano ya wanazuoni. Vivyo hivyo swalah ya wale walioko nyuma yake kwa mujibu wa maoni sahihi zaidi ya wanazuoni. Lakini kafiri swalah yake haisihi wala ya wale walioko nyuma yake kwa kukosekana sharti yake ambayo ni Uislamu.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa Muhimmah, uk. 60