Swali 55: Imamu amewaswalisha maamuma pasi na wudhuu´ kwa kusahau. Ni ipi hukumu ya swalah hii katika hali zifuatazo:

1 – Akikumbuka jambo hilo katikati ya swalah?

2 – Akikumbuka baada ya salamu na kabla ya watu kuondoka?

3 – Akikumbuka baada ya watu kutawanyika?

Jibu: Akikumbuka baada ya kutoa salamu basi swalah ya maamuma ni sahihi na si lazima kwao kuirudia. Lakini imamu yeye atalazimika kuirudia.

Lakini akikumbuka katikati ya swalah basi anatakiwa kuteua ambaye atawakamilishia swalah yao kwa mujibu wa maoni sahihi zaidi ya wanazuoni. Hilo ni kutokana na kisa cha ´Umar (Radhiya Allaahu ´anh) wakati alipodungwa ndani ya swalah alimteua ´Abdur-Rahmaan bin ´Awf (Radhiya Allaahu ´anh) ambapo akawakamilishia swalah na hakuianza mwanzo.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa Muhimmah, uk. 59-60
  • Imechapishwa: 07/09/2022