Swali: Kuna makundi mengi katika ulimwengu wetu wa Kiislamu na wa kiarabu ambayo hawana shughuli nyingine isipokuwa kuhimiza kuingia bungeni kupitia njia ya uchaguzi. Unatushauri nini?

Jibu: Maisha ya kibunge msingi wake ni wa kimagharibi, kiajemi na yasiyokuwa ya kiislamu. Mbunge anafika bungeni kupitia uchaguzi. Tunajua namna unavyokuwa uchaguzi. Hata kama wanaita kuwa ni uchaguzi huru na uchaguzi msafi, itambulike kuwa hakuna uchaguzi huru wala msafi. Inahusiana na kununua kura, mapendeleo, kupakana mafuta na mengine mengi. Ni mambo yanayojulikana.

Inapotokea mtu amechaguliwa kama mbunge, basi anatakiwa kuapa kuheshimu kanuni. Kanuni hiyo sio ya Kiislamu. Ni kanuni ya kisekula. Endapo utamuuliza mbunge huyu kama bunge lao hili lina utawala unaotunga sheria au kutekeleza hukumu, atasema kuwa ni utawala unaotunga sheria. Kwa msemo mwingine ni utawala unaoshirikiana na kushindana na Allaah kutunga sheria. Je, inafaa kwa muislamu kujiita kuwa ni mtunga sheria? Wajumbe wa leo wanaitwa watunga sheria na wajumbe katika kamati ya kutunga sheria. Unatunga sheria gani?

Je, hatutosheki na Shari´ah iliyowekwa na Allaah? Shari´ah yote ya Allaah imo ndani ya Qur-aan. Tukitunga sheria inayoenda kinyume na Shari´ah ya Allaah, hiyo maana yake ni kwamba hatukuridhia Shari´ah ya Allaah. Kwa hivyo mabunge kama hayo mosi yanakufuru na kukichezea shere Kitabu cha Allaah. Haijuzu kwa muislamu, anayeheshimu imani yake, kushiriki katika mabunge ya leo. Bunge siku zote ni bunge ingawa nchi za bunge zinaweza kutofautiana katika kufanyia kwao kazi demokrasia. Mara nyingi wote hufanyia kazi demokrasia. Demokrasia maana yake raia ndio wenye kuhukumu. Kwa maana nyingine ni kwamba wanaipa mgongo hukumu ya Allaah na dini Yake kwa ajili ya kuhukumu wenyewe kwa wao wenyewe. Wanaona kuwa hukumu ya Allaah ambayo ndani yake kuna kufanya kisasi, kukata mkono na kuchapa bakora migongo ni hukumu zenye ususuwavu zisizoendana na ulimwengu huu ulioendelea. Ulimwengu huu ulioendelea unahitaji hukumu nyumbufu ambazo zitawepesisha hukumu hizi zenye ususuwavu. Kwa hivyo badala ya kisasi watunge sheria ya kifungo cha milele. Baada ya hapo hukumu inasema hukumu ya kifungo cha milele ipunguzwe kifungo cha miaka kumi. Baada ya siku kadhaa unamuona yule ambaye kamuua baba yako anatembea mbele yako, kwa sababu kanuni imemruhusu kumtoka nje. Je, huku si ni kucheza na Kitabu cha Allaah? Je, huku si ni kukufuru hukumu ya Allaah? Jambo liko wazi sana. Hakuna haja ya makinzano.

  • Mhusika: ´Allaamah Muhammad Amaan bin ´Aliy al-Jaamiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://www.youtube.com/watch?app=desktop&v=YgtzqzNjlIU
  • Imechapishwa: 07/09/2022