Wanachuoni wametofautinaa katika kuelezea maana ya ´ibaadah ya Kishari´ah. Kwa msemo ibara zao zimetofautiana katika kuiarifisha japo maana ni moja. Miongoni mwao wamesema kuwa ´ibaadah ni ule upeo wa kujidhalilisha na upeo wa mapenzi. Hayo yamesememwa na Ibn-ul-Qayyim katika “an-Nuuniyyah” yake:

´Ibaadah ya Mwingi wa huruma ni upeo wa mapenzi

pamoja na kujidhalilisha kwa mja Wake – viwili hivyo ni nguzo mbili

Akaeleza kuwa ni ule upeo wa mapenzi na upeo wa kujidhalilisha.

Wengine wakasema kuwa ´ibaadah ni yale yaliyoamrishwa Kishari´ah pasi na kuzingatia kidesturi wala kwamba akili imepelekea hivo. Kwa sababu ´ibaadah ni kitu cha kukomeka na wala haithibiti kwa akili wala kwa desturi. Bali inathibiti kwa akili. Maana hii ni sahihi.

Lakini maana iliyoenea na iliyokusanya ni ile aliyoelezea Shaykh-ul-Islaam Ibn Taymiyyah (Rahimahu Allaah) pale aliposema:

“´Ibaadah ni neno lililokusanya kila kile anachokipenda Allaah na kukiridhia katika maneno na matendo, yenye kuonekana na yaliyojificha.”

Maana hii imekusanya na imeenea. ´Ibaadah ni neno lililokusanya yale yote aliyoamrisha Allaah. Kufanya yale yote aliyoamrisha Allaah hali ya kumtii Allaah na kuacha yale yote aliyokataza Allaah hali ya kumtii Allaah. Hii ndio ´ibaadah. Hazifupiki aina zake. Aina zake ni nyingi. Kila alichoamrisha Allaah ni ´ibaadah. Kuacha kila alichokataza Allaah hali ya kumtii Allaah ni ´ibaadah. Hazifupiki aina zake. Aina zake ni nyingi. Kila alichoamrisha Allaah ni ´ibaadah. Kila alichokataza Allaah mtu anatakiwa kukiacha. Ni mamoja kitu hicho kinaonekana katika viungo vya mwili au kiko ndani ya moyo. Kwa sababu ´ibaadah inakuwa kupitita mdomo, moyo na viungo vya mwili.

´Ibaadah inakuwa kupitia mdomo kama mfano wa kusema “Subhaan Allaah”, Dhikr, kusema “Laa ilaaha illa Allaah” na shahaadah. Maneno yote yaliyowekwa katika Shari´ah katika kumtaja Allaah (´Azza wa Jall) ni ´ibaadah.

Vivyo hivyo kila kilichomo ndani ya moyo katika kujikurubisha kwa Allaah (´Azza wa Jall) ni ´ibaadah. Kwa mfano wa khofu, kutaraji, tisho, kuogopa, shauku, kutegemea, kurejea na kutaka msaada kwa Allaah. Yote haya ni matendo ya moyo. Kumwelekea Allaah kimoyo, kumcha Allaah, kumwogopa, kuwa na shauku Naye, kumwogopa, kumpenda Yeye (Subhaanah), kumtakasia Yeye nia na nia ya kweli kwa Allaah (´Azza wa Jall). Kila kilichomo moyoni katika aina hizi ni ´ibaadah.

Vivyo hivyo ´ibaadah inakuwa kupitia viungo vya mwili kama mfano wa kurukuu, sujudu, kupambana jihaad katika njia ya Allaah, kupambana jihaad kwa nafsi na kuhajiri. Zote hizi ni ´ibaadah za kimwili. Kadhalika kufunga ni ´ibaadah ya kimwili inayoonekana katika viungo vya mwili.

Kwa hivyo ´ibaadah inakuwa kupitia mdomo, moyo na viungo vya mwili.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Thalaathat-il-Usuwl, uk. 122-124
  • Imechapishwa: 22/12/2020