55. Nyimbo za kidini – njia ya kuwatega watu wa kawaida

Ni uzuri uliyoje wa maneno ya Shaykh-ul-Islaam (Rahimahu Allaah) pale aliposema nyimbo hizi zilizozuliwa ni mtandao ambao wanategwa kwao watu wajinga! Amesema kweli. Wengi wao wanazichukulia nyimbo kwa ajili ya kutaka kusakata tonge. Ambaye anafanya hivo ni miongoni mwa viongozi wa wapotofu ambao imesemwa juu yao:

يَوْمَ تُقَلَّبُ وُجُوهُهُمْ فِي النَّارِ يَقُولُونَ يَا لَيْتَنَا أَطَعْنَا اللَّـهَ وَأَطَعْنَا الرَّسُولَا وَقَالُوا رَبَّنَا إِنَّا أَطَعْنَا سَادَتَنَا وَكُبَرَاءَنَا فَأَضَلُّونَا السَّبِيلَا رَبَّنَا آتِهِمْ ضِعْفَيْنِ مِنَ الْعَذَابِ وَالْعَنْهُمْ لَعْنًا كَبِيرًا

”Siku zitakapopinduliwa nyuso zao Motoni, watasema ”Ee laiti tungelimtii Allaah na tungelimtii Mtume. Na watasema ”Ee Mola wetu! Hakika sisi tuliwatii mabwana zetu na wakuu wetu wakatupoteza njia. Ee Mola wetu! Wape adhabu maradufu na walaani laana kubwa”.”[1]

Hata wale wajinga katika wao ambao ni wakwelihuzitumia kama mtandao, lakini ni mtandao uliotoboka na huchomoka yule anayetumbukia ndani yake haraka tu anavyoingia. Hayo hutokea mara nyingi kikweli. Wale ambao huingia katika nyimbo zilizozuliwa hawana msingi wa Shari´ah uliowekwa na Allaah na Mtume Wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Aidha hutumbukia katika hali mbovu[2]. Hayo ndio matokeo ya mifumo iliyozuliwa. Mbaya juu ya mbaya, giza juu ya giza.

[1] 33:66-68

[2] Tazama ”Majmuu´-ul-Fataawaa” (11/601).

  • Mhusika: Shaykh ´Abdus-Salaam bin Barjas Aal ´Abdil-Kariym
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Hujaj al-Qawiyyah ´alaa anna Wasaa-il-ad-Da´wah Tawqiyfiyyah, uk. 80-81
  • Imechapishwa: 28/05/2023