Inajuzu kusoma Qur-aan kwa visomo saba vilivyokubaliwa kwa maafikiano. Haijuzu kusoma kwa visomo visivyo hivyo saba. Wala haijuzu kusoma kwa visomo visivyo sahihi vilivyopokelewa kutoka kwa wasomaji wengine visivyokuwa vile saba. Itakuja katika mlango wa saba maelezo ya maafikiano ya wanazuoni juu ya kumtaka atubie yule anayefundisha visomo visivyo sahihi au akavisoma.
Wamesema maswahiba wetu na wengine kwamba ikiwa mtu atasoma kwa visomo visivyo sahihi ndani ya swalah, basi swalah yake itabatilika ikiwa anajua. Ikiwa hajui, basi haitabatilika. Lakini kisomo hicho hakitahesabiwa kwake.
Imaam na Haafidhw Abu ´Umar bin ´Abdil-Barr (Rahimahu Allaah) amenukuu maafikiano ya waislamu kwamba haijuzu kusoma kwa visomo visivyo sahihi na kwamba hakuswaliwi nyuma ya yule anayevisoma. Wanazuoni wamesema kwamba anayesoma kwa visomo visivyo sahihi ikiwa hajui hukumu ya uharamu wake, basi afundishwe hilo. Akirudia baada ya kuelimishwa au ikiwa alikuwa anajua, basi aadhibiwe kwa adhabu kali ya nidhamu mpaka aache kitendo hicho. Ni wajibu kwa kila mwenye uwezo wa kumkemea na kumzuia kufanya hivyo kadiri ya uwezo wake – Allaah ndiye Mjuzi zaidi.
- Muhusika: Imaam Yahyaa bin Sharaf an-Nawawiy (afk. 677)
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: at-Tibyaan fiy Aadaabi Hamalat-il-Qur-aan, uk. 61
- Imechapishwa: 02/09/2026
Inajuzu kusoma Qur-aan kwa visomo saba vilivyokubaliwa kwa maafikiano. Haijuzu kusoma kwa visomo visivyo hivyo saba. Wala haijuzu kusoma kwa visomo visivyo sahihi vilivyopokelewa kutoka kwa wasomaji wengine visivyokuwa vile saba. Itakuja katika mlango wa saba maelezo ya maafikiano ya wanazuoni juu ya kumtaka atubie yule anayefundisha visomo visivyo sahihi au akavisoma.
Wamesema maswahiba wetu na wengine kwamba ikiwa mtu atasoma kwa visomo visivyo sahihi ndani ya swalah, basi swalah yake itabatilika ikiwa anajua. Ikiwa hajui, basi haitabatilika. Lakini kisomo hicho hakitahesabiwa kwake.
Imaam na Haafidhw Abu ´Umar bin ´Abdil-Barr (Rahimahu Allaah) amenukuu maafikiano ya waislamu kwamba haijuzu kusoma kwa visomo visivyo sahihi na kwamba hakuswaliwi nyuma ya yule anayevisoma. Wanazuoni wamesema kwamba anayesoma kwa visomo visivyo sahihi ikiwa hajui hukumu ya uharamu wake, basi afundishwe hilo. Akirudia baada ya kuelimishwa au ikiwa alikuwa anajua, basi aadhibiwe kwa adhabu kali ya nidhamu mpaka aache kitendo hicho. Ni wajibu kwa kila mwenye uwezo wa kumkemea na kumzuia kufanya hivyo kadiri ya uwezo wake – Allaah ndiye Mjuzi zaidi.
Muhusika: Imaam Yahyaa bin Sharaf an-Nawawiy (afk. 677)
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: at-Tibyaan fiy Aadaabi Hamalat-il-Qur-aan, uk. 61
Imechapishwa: 02/09/2026
https://firqatunnajia.com/55-kusoma-qur-aan-kwa-aina-saba-ya-visomo/