54. Kisono cha Qur-aan kwa lugha isiyo ya kiarabu

Haijuzu kusoma Qur-aan kwa lugha isiyo ya kiarabu, ni mamoja iwe mtu anajua kiarabu au hajui, ni mamoja iwe ndani ya swalah au nje ya swalah. Ikiwa atasoma kwa lugha hiyo ndani ya swalah, basi swalah yake haisihi. Haya ndiyo maoni yetu, Maalik, Ahmad, Daawuud na Abu Bakr bin al-Mundhir.

Abu Haniyfah amejuzisha kitendo hicho na akasema kuwa swalah inasihi kwa kufanya hivo.

Abu Yuusuf na Muhammad wamejuzisha kitendo hicho kwa yule asiyejua kiarabu na haijuzu kwa yule anayejua kiarabu.

  • Muhusika: Imaam Yahyaa bin Sharaf an-Nawawiy (afk. 677)
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: at-Tibyaan fiy Aadaabi Hamalat-il-Qur-aan, uk. 61
  • Imechapishwa: 02/09/2026