54. Hadiyth ”Hawatokaa watu kikao ambacho… ”

54 – Muhammad bin Kathiyr ametuhadithia: Sufyaan bin Sa´iyd, kutoka kwa Swaalih, mtumwa wa at-Taw-amah aliyemwacha huru, kutoka kwa Abu Hurayrah, aliyesimulia kuwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

ما جلس قوم مجلساً لم يذكروا الله، ولم يصلوا على نبيهم صلى الله عليه وسلم، إلا كان مجلسهم عليهم ترة يوم القيامة، إن شاء عفا عنهم، وإن شاء أخذهم

”Hawatokaa watu kikao ambacho wasimtaje Allaah na wala hawaswalii Mtume wao (Swalla ´alayhi wa sallam), isipokuwa kikao chao hicho kitakuwa ni majuto siku ya Qiyaamah; akitaka kuwasamehe atawasamehe, na akitaka kuwachukulia hatua atawachukulia hatua.”[1]

[1] Hadiyth ni Swahiyh. Wapokezi wake wote ni waaminifu, isipokuwa Swaalih, mtumwa wa at-Taw-amah aliyemwacha huru, ni mnyonge kwa sababu ya kuchanganyikiwa kwake. Hata hivyo hakuisilimua peke yake. Bali alifuatwa na Abu Swaalih as-Simaan Dhakwaan, Sa´iyd bin Abiy Sa´iyd al-Maqburiy na Abu Ishaaq, mtumwa aliyeachwa huru na al-Haarith, kutoka kwa Abu Hurayrah, kwa matamshi yanayokaribiana. Nimeitaja katika “Silsilat-ul-Ahaadiyth as-Swahiyhah” (73-78), kwa hivyo rejea huko.

  • Mhusika: Imaam Ismaa´iyl bin Ishaaq al-Maalikiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fadhwl-us-Swalaah ´alaan-Nabiy, uk. 53
  • Imechapishwa: 22/01/2024
  • taaliki: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy