53. Hadiyth ”Mwenye kusema: ´Ee Allaah! Mswalie Muhammad… ”

53 – Yahyaa ametuhadithia: Zayd bin Habbaab ametuhadithia: Ibn Lahiy´ah amenikhabarisha: Bakr bin Sawaadah al-Mu´aafiriy amenihadithia, kutoka kwa Ziyaad bin Nu´aym al-Hadhwramiy, kutoka kwa Ibn Shurayh: Ruwayfiy´ al-Answaariy amenihadithia ya kwamba amemsikia Mtume (Swaalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

من قال: اللهم صلي على محمد، وأنزله المقعد المقرب منك يوم ا”لقيامة، وجبت له الشفاعة

”Mwenye kusema: ´Ee Allaah! Mswalie Muhammad na mkaze karibu Nawe siku ya Qiyaamah!` basi umemthubutikia uombezi wangu.”[1]

[1] Cheni ya wapokezi ni dhaifu kwa sababu ya Abu Lahiy´ah ambaye jina lake ni ´Abdullaah. Ameipokea al-Bazzaar na at-Twabaraaniy katika “al-Mu´jam al-Awsatw”. al-Mundhiriy na al-Haythamiy wamesema kuwa cheni za wapokezi wake ni nzuri. Nadhani kuwa ni kupitia njia ya Ibn Lahiy´ah. Mambo yakiwa hivo, basi kuifanya kuwa ni nzuri ni jambo linatakiwa kuangaliwa vizuri. Kisha baadaye nikajihakikishia jambo hilo pindi niliposoma katika “Jalaa’-ul-Afhaam”, uk. 56, ya Ibn-ul-Qayyim namna ambavyo at-Twabaraaniy ameisimulia Hadiyth kupitia njia hii.

  • Mhusika: Imaam Ismaa´iyl bin Ishaaq al-Maalikiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fadhwl-us-Swalaah ´alaan-Nabiy, uk. 52-53
  • Imechapishwa: 22/01/2024
  • taaliki: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy