Kuna aina mbili za upamoja wa Allaah (المعية) na viumbe Wake:

1 – Upamoja wenye kuenea kwa muumini na kafiri. Allaah yuko pamoja na waumini na makafiri kwa kuwaona, kuwachunga na kupitisha uwezo na matakwa Yake:

وَهُوَ مَعَكُمْ أَيْنَ مَا كُنتُمْ وَاللَّهُ بِمَا تَعْمَلُونَ بَصِيرٌ

”Naye Yu Pamoja nanyi popote mlipo. Na Allaah kwa myatendayo ni Mwenye kuyaona.”[1]

2 – Upamoja maalum kwa waumini na Mitume. Amesema (Ta´ala):

إِنَّ اللَّـهَ مَعَ الَّذِينَ اتَّقَوا وَّالَّذِينَ هُم مُّحْسِنُونَ

“Hakika Allaah Yu Pamoja na wenye kumcha na wale watendao wema.”[2]

Kwa hivyo Yeye yuko pamoja na wenye kumcha na pamoja na wafanyao wema kwa kuwanusuru, kuwatia nguvu, kuwawafikisha, kuwafanya imara na wakati huohuo yuko juu ya ´Arshi. Allaah (Ta´ala) amesema kuhusu Muusa na Haaruun:

قَالَ لَا تَخَافَا ۖ إِنَّنِي مَعَكُمَا أَسْمَعُ وَأَرَىٰ

“Hakika Mimi Niko pamoja nanyi, Nasikia na Naona.”[3]

Amesema kuhusu Mtume wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) wakati alipokuwa katika pango la Hiraa´ pamoja na Abu Bakr as-Swiddiyq (Radhiya Allaahu ´anh):

لاَ تَحْزَنْ إِنَّ اللّهَ مَعَنَا

“Usihuzunike – hakika Allaah Yu Pamoja nasi!”[4]

[1] 57:04

[2] 16:128

[3] 20:46

[4] 09:40

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Thalaathat-il-Usuwl, uk. 81
  • Imechapishwa: 14/02/2023