Shaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab (Rahimahu Allaah) amesema:

Ngazi ya tatu: Ni Ihsaan. Ina nguzo moja, nayo ni kumwabudu Allaah kama vile unamuona. Ikiwa wewe humuoni, basi Yeye anakuona[1].

Dalili ya ni Kauli Yake (Ta´ala):

إِنَّ اللَّـهَ مَعَ الَّذِينَ اتَّقَوا وَّالَّذِينَ هُم مُّحْسِنُونَ

“Hakika Allaah yupamoja na wenye kumcha na wale watendao wema.”[2]

وَتَوَكَّلْ عَلَى الْعَزِيزِ الرَّحِيمِ الَّذِي يَرَاكَ حِينَ تَقُومُ وَتَقَلُّبَكَ فِي السَّاجِدِينَ إِنَّهُ هُوَ السَّمِيعُ الْعَلِيمُ

”Tegemea kwa Mwenye nguvu kabisa asiyeshindika, Mwenye kurehemu, ambaye anakuona wakati unaposimamama, na mageuko yako na wenye kusujudu. Hakika Yeye ni Mwenye kusikia, Mjuzi wa yote.”[3]

وَمَا تَكُونُ فِي شَأْنٍ وَمَا تَتْلُو مِنْهُ مِن قُرْآنٍ وَلَا تَعْمَلُونَ مِنْ عَمَلٍ إِلَّا كُنَّا عَلَيْكُمْ شُهُودًا إِذْ تُفِيضُونَ فِيهِ

“Hushughuliki katika jambo lolote wala husomi humo chochote katika Qur-aan na wala hamtendi ‘amali yoyote isipokuwa Tunakuwa ni mashahidi juu yenu mnaposhughulika nayo.”[4]

MAELEZO

Hii ndio ngazi ya tatu miongoni mwa zile ngazi za dini; ihsaan. Ina nguzo moja wakati Uislamu una tano na imani ina nguzo tano. Huku ndio kuchunga ambapo unatakiwa kumwabudu Allaah hali ya kujua kuwa anakuona, kitu ambacho ndio ukamilifu wa imani.

 Nguzo hii ina ngazi mbili ambapo ngazi ya kwanza iko juu zaidi kuliko ngazi ya kwanza:

1 – Unamwabudu Allaah kama kwamba unamuona mbele Yako. Ukidhoofika kutokana na ngazi hii unahamia kwenda katika ya pili:

2 – Ikiwa wewe humuoni basi utambue kuwa Yeye anakuona. Kwa msemo mwingine ni kwamba umwabudu Allaah kujengea ya kwamba anakuona.

Mtu ambaye anamwabudu Allaah kujengea ya kwamba anamuona anaweza kujionyesha katika matendo yake? Kimaumbile ni kwamba hawezi kufanya hivo. Anayemwabudu katika hali hiyo utamuona anamtakasia nia Allaah na wala moyo wake hauwaeukii watu.

Maneno Yake (Ta´ala):

إِنَّ اللَّـهَ مَعَ الَّذِينَ اتَّقَوا وَّالَّذِينَ هُم مُّحْسِنُونَ

“Hakika Allaah yupamoja na wenye kumcha na wale watendao wema.”

Huu ni upamoja wa nusura, kuwatia nguvu, kuwawafikisha na kuwafanya imara.

[1] al-Bukhaariy (09).

[2] 16:128

[3] 26:217-220

[4] 10:61

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Thalaathat-il-Usuwl, uk. 80-81
  • Imechapishwa: 14/02/2023