51. Tofauti kati ya nguzo za Uislamu na nguzo za imani

1 – Nguzo za Uislamu ni shahaadah mbili, swalah, zakaah, swawm na hajj. Hizi ndio nguzo za Uislamu. Ni nguzo zilizo dhahiri.

2 – Kuhusu nguzo za imani ni matendo yaliyojificha. Hakuna anayezijua isipokuwa Allaah pekee. Yule mwenye kuamini nguzo za imani zilizojificha ni muumini na ambaye ataamini nguzo za Uislamu za dhahiri na asiamini nguzo za imani zilizojificha ni mnafiki na atakuwa katika tabaka la chini kabisa Motoni.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Thalaathat-il-Usuwl, uk. 79
  • Imechapishwa: 14/02/2023