Maneno Yake (Ta´ala):

أَلَا لَهُ الْخَلْقُ وَالْأَمْرُ

”Tanabahi! Ni Vyake pekee uumbaji na amri.”

Tanabahi! – Ni chombo cha kuzindua.

Ni Vyake – Yeye (Subhaanahu wa Ta´ala) na si vya mwengine.

Uumbaji – Yeye ni muweza wa kuumba anapotaka (Subhaanahu wa Ta´ala) anaumba anachotaka.

Amri – Amri Yake (Subhaanahu wa Ta´ala). Nayo ni yale maneno Yake (Subhaanahu wa Ta´ala) ya kilimwengu na ya Kishari´ah.

Amri ya kilimwengu ni ile anayowaamrisha kwayo viumbe ambapo wakamtii na wakamwitikia. Mfano wa maneno Yake:

فَقَالَ لَهَا وَلِلْأَرْضِ ائْتِيَا طَوْعًا أَوْ كَرْهًا

“Akaziambia hizo na ardhi “Njooni kwa kutaka kwenu au pasi na kutaka.“[1]

Amri Yake kwa wili hivyo (Subhaanahu wa Ta´ala). Hii ni amri Yake ya kilimwengu ambayo ameziamrisha mbingu na ardhi na ikawa hivyo:

إِنَّمَا أَمْرُهُ إِذَا أَرَادَ شَيْئًا أَن يَقُولَ لَهُ كُن فَيَكُونُ

”Hakika amri Yake anapotaka chochote hukiambia: “Kuwa!” nacho huwa.”[2]

Hii ni amri Yake ya kilimwengu.

Amri Yake ya Kishari´ah ni ule Wahy Wake uliyoteremshwa ambao amewaamrisha kwao waja Wake. Anawaamrisha wamwabudu Yeye kama mfano wa kuswali, kutoa zakaah na kuwatendea wema wazazi. Hii ni amri Yake ya Kishari´ah ambayo kunaingia ndani yake maamrisho na makatazo yaliyomo ndani ya Qur-aan na Sunnah za Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Haya ni katika amri ya Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala). Ikiwa uumbaji na amri ni Yake kumebaki nini kwa wengineo asiyekuwa Yeye (Subhaanahu wa Ta´ala)? Kwa ajili hii Ibn ´Umar, wakati aliposoma Aayah hii, alisema:

“Yule mwenye jambo aliombe.”

Aayah pia imefahamisha utofauti kati ya uumbaji na amri. Kuna Radd kwa wale wanaosema kuwa Qur-aan imeumbwa. Kwa sababu Qur-aan ni katika amri. Amri ya Allaah haikuumbwa kwa sababu Allaah ametofautisha kati ya uumbaji na amri. Amefanya ni vitu viwili tofauti. Qur-aan inaingia ndani ya amri na hivyo haikuumbwa. Haya ni miongoni mwa mambo ambayo Imaam Ahmad aliwagombeza Jahmiyyah wakati walipomtaka aseme kuwa Qur-aan imeumbwa. Akasema kuwauliza: “Je, Qur-aan ni katika uumbaji au ni katika amri?” Wakasema: “Qur-aan ni katika amri.” Ndipo akasema: “Amri haikuumbwa. Allaah ametofautisha kati ya amri na uumbaji ambapo akafanya uumbaji ni kitu kimoja na amri ni kitu kingine.” Amri ni maneno. Ama uumbaji ni utengenezaji. Kwa hiyo kuna tofauti kati ya hayo mawili.

“tabaraka Allaah”

Bi maana ametukuka Ambaye haya ndio matendo Yake (Subhaanahu wa Ta´ala), huu ndio uwezo Wake na huu ndio uumbaji Wake (Tabaarak wa Ta´ala).

Kubarikika ni kitendo maalum cha Allaah. Haisemwi juu ya mwengine. Baraka ni wingi wa kheri na ukuaji wake. Baraka za Allaah (Jalla wa ´Alaa) hazina mwisho. Haisemwi kubarikika juu ya viumbe. Viumbe wanaambiwa kuwa ni wenye kubarikiwa. Kwa msemo mwingine kwamba Allaah amewabariki na amewafanya kuwa ni wenye baraka. Baraka zote ni kutoka kwa Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala).

Mola wa walimwengu – Ni kama tulivyotangulia kutaja.

Katika Aayah hizi kumethibitishwa kwa Tawhiyd; Tawhiyd-ul-Uluuhiyyah na Tawhiyd-ur-Rubuubiyyah kama tulivyotangulia kutaja.

[1] 41:11

[2] 36:82

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Thalaathat-il-Usuwl, uk. 116-118
  • Imechapishwa: 21/12/2020