1- Ibraahiym bin Sa´iyd al-Jawhariy amesema:

“Nilimuona mvulana wa miaka mine amepelekwa kwa al-Ma´muun. Kijana huyo alikuwa amehifadhi Qur-aan, ameyasoma vizuri maoni, lakini anapokuwa na njaa basi analia.”[1]

2- Abu Muhammad bin al-Labbaan amesema:

“Nilihifadhi Qur-aan pindi nilipokuwa na miaka tano.”[2]

3- az-Zubayr bin Bakkaar amesema:

“Msichana wa dada yangu alisema kumwambia mke wangu: “Mjomba wangu ni mume bora kabisa; hana mke mwingine wala mjakazi.” Ndipo mwanamke akasema: “Ninaapa kwa Allaah! Vitabu hivi ni vizito zaidi kwangu kuliko wake watatu wa majirani.”[3]

4- Muhammad bin Ishaaq as-Swayrafiy amesema:

“Nilimuuliza az-Zubayr: “Ni muda kiasi gani uliishi na mke wako?” Akajibu: “Usiniulize. Hakuna yeyote atakayekuja siku ya Qiyaamah na kondoo wengi wa kiume kuliko yeye. Nimemchinjia kondoo sabini wa kiume.”[4]

5- Rajaa´ al-Haafidhw amesema:

“Ubora wa Muhammad bin Ismaa´iyl juu ya wanachuoni ni kama ubora wa mwanamme juu ya wanawake.” Mtu mmoja akamwambia: “Ee Abu Muhammad! Kweli ndivo?” Akajibu: “Yeye ni alama miongoni mwa alama za Allaah juu ya ardhi.”[5]

6- ´Abdullaah bin Muammad as-Swaarifiy amesema:

“Nilikuwa nyumbani kwa Abu ´Abdillaah kipindi ambapo mjakazi wake alikuja na akataka kuingia ndani ya nyumba ambapo akajikwaa kwenye wino uliokuwa mbele yake. Akasema: “Utatembea vipi?” Mjakazi yule akasema: “Nitatembea vipi ikiwa hakuna njia?” Akanyoosha mikono yake na kumwambia: “Nenda zako! Hakika nimekuacha huru.” Baadaye akaulizwa kama kijakazi yule kamkasirisha ambapo akajibu: “Hata kama atakuwa amenikasirisha mimi nimeridhia kitendo nilichokifanya.”[6]

[1] Siyar A´laam-in-Nubalaa’ (12/150).

[2] Siyar A´laam-in-Nubalaa’ (12/150).

[3] Siyar A´laam-in-Nubalaa’ (12/313).

[4] Siyar A´laam-in-Nubalaa’ (12/314).

[5] Siyar A´laam-in-Nubalaa’ (12/427).

[6] Siyar A´laam-in-Nubalaa’ (12/452).

  • Mhusika: Imaam Shams-ud-Diyn Muhammad bin Ahmad adh-Dhahabiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Siyar A´laam-in-Nubalaa’
  • Imechapishwa: 21/12/2020