52. Bora na salama zaidi kwa msafiri akinuia kukaa katika mji zaidi ya siku nne

Swali 52: Nikiwa msafiri Ramadhaan na sikufunga safarini mwangu na wakati nitapofika katika ule mji ambao nitakaa kwa muda wa masiku kadhaa nitajizuilia kufunga masaa yaliyobaki ya siku hiyo na masiku mengine yanayofuata. Je, nina ruhusa ya kula michana ya masiku haya ilihali niko katika nchi ambayo siyo ile yangu ya asili[1]?

Jibu: Msafiri akipita katika nchi isiyokuwa nchi yake ilihali ni mwenye kula, basi hahitajii kujizuilia ikiwa kukaa kwake ni kwa muda usiyozidi siku nne. Lakini akiwa amenuia kukaa ndani yake zaidi ya siku nne, basi atajizuilia siku hiyo ambayo amefika hali ya kuwa ni mwenye kula na atailipa baadaye. Aidha atalazimika kufunga masiku mengine yaliyobaki. Kwa sababu kutokana na nia yake iliyotajwa amekuwa na hukumu moja kama wakazi na si mwenye hukumu kama wasafari kwa mtazamo wa wanazuoni wengi.

[1] Majmuu´-ul-Fataawaa (15/244).

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Ahkaam-ul-Musaafir, uk. 69
  • Imechapishwa: 20/05/2022