Manufaa ya Jamaa´at-ut-Tabliygh ni kama manufaa ya pombe

Hawa ambao wanalingania katika Uislamu – je, wanaujua Uislamu?

Muulizaji: Hapana.

al-Albaaniy: Kwa hivyo wanalingania katika kitu gani? Wanalingania katika kitu gani? Wanatakiwa kukaa majumbani mwao katika miji yao na wasome. Kwa sababu asiyekuwa na kitu hakuna awezacho kutoa. Kama nilivosema tangu hapo kitambo na bado nasema vivyo hivyo na nitaendelea kusema hivo huko mbeleni sana isipokuwa ikiwa watabadilika, Jamaa´at-ut-Tabliygh ni Suufiyyah wa sasa. Suufiyyah siku zote imejengeka juu ya ujinga kuhusu Uislamu. Kwa ajili hiyo wamewadhuru waislamu zaidi kuliko walivowanufaisha. Ninaposema kuwa wamedhuru zaidi kuliko walivonufaisha, mnachopata kufahamu vyema ni kwamba wananufaisha. Wanazuoni na watu wengi wenye kuheshimiwa wanaangalia upande huu na wanafumbia macho upande mwingine, nao ni kwamba wanadhuru zaidi kuliko wanavonufaisha. Wakati Mola wetu (´Azza wa Jall) alipoharamisha pombe alisema kuwa ndani yake mna manufaa kwa watu, lakini madhara na dhambi zake ni kubwa zaidi kuliko manufaa yake.

Kwa hiyo haijuzu kwa yeyote kuwafanyia kampeni Jamaa´at-ut-Tabliygh kutokana na yale mazuri yanayodhihiri kwao katika baadhi ya nyanja na baadhi ya watu. Badala yake ni lazima kwetu kutazama malengo ya ulinganizi huu ambao umejengeka juu ya ujinga juu ya Uislamu. Suufiyyah katika nyakati zote inanufaisha, lakini manufaa yake ni kama pombe iliyoharamishwa. Inanufaisha, lakini wana mabaya na maovu mengi.

  • Mhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa Juddah (8)
  • Imechapishwa: 20/05/2022