Swali: Ni yepi maoni yako kuhusu Ummah wa Da´wah?

Jibu: Hili ni jina jipya kwangu, lakini nadhani unakusudia lile jina la zamani; Jamaa´at-ut-Tabliygh.

Mimi bado sijakinaika kuwa Jamaa´at-ut-Tabliygh ni kipote – na himdi zote njema anastahiki Allaah.

Upande wa pili bado sijakinaika kuwa ndio kipote Kilichonusuriwa (at-Twaaifah al-Mansuurah). Kwa nini? Kwa sababu hawatendei kazi Sunnah.

Muulizaji: Hawatendei kazi?

al-Albaaniy: [Hawatendei kazi] Sunnah. Kuta zina masikio au?

Muulizaji: Inakuweje hivo ilihali wanaanza mawaidha yao kwa kusema:

“Uokozi wetu na kufaulu kwetu duniani na Aakhirah ni kwa kufuata maamrisho ya Allaah na Sunanh za Mtume.”?

al-Albaaniy: Nataka kurudi kwa Shaykh kwa sababu yeye ndiye ambaye ameanza mawaidha yake kwa mneno hayo. Ningepeda kukumbusha kwamba hakuna kati yetu sisi na kundi jingine lolote usumbufu wowote. Sababu ya hilo ni kwa kuwa ulinganizi wetu ni wenye kuenea zaidi ulimwenguni kote. Baadhi ni al-Ikhwaan al-Muslimuun, wengine ni Hizb-ut-Tahriyr, wengine ni Jamaa´at-ut-Tabliygh na kadhalika. Sisi tunasema kwamba tunafata yale yaliyosemwa na Allaah na yaliyosemwa na Mtume Wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Ni muislamu yupi ambaye anaweza kujitenga mbali na ulinganizi wetu? Hakuna yeyote. Lakini wako wengi wanaofanya hivo. Sikiliza maneno haya yanayojigonga kisha yaoanishe. Hakuna yeyote awezaye kwenda kinyume na ulinganizi wetu. Lakini wengi wanafanya hivo. Hawaendi kinyume na sisi kwa kusema waziwazi, lakini wanafanya hivo kimatendo, kimfumo na kiutendaji kazi.

Hebu wacha tuanze kwa swali lako. Sisi tunawakosoa Jamaa´at-ut-Tabliygh kwa utangulizi huu ambao siku zote wanaanza nao mwanzoni mwa mwa mawaidha yao yote. Pamoja na kwamba nimeshakuwa mzee, sijawahi kuwasikia hata siku moja wakianza mawaidha yao kwa Khutbah ya Haajah. Je, haya si katika Sunnah? Hapana shaka, lakini hawatilii umuhimu jambo la Sunnah.

Nimefikiwa na khabari za ukweli ya kwamba walikuwa – lakini wameanza kujifunza, lakini si kutoka kwao wenyewe, isipokuwa ni kutoka kwa wale wenye kushikamana na ulinganizi wa haki, nao ni ulinganizi wa Qur-aan na Sunnah. Ni kama ambavo al-Ikhwaan al-Muslimuun nao wameanza kujifunza, lakini si kutoka kwao wenyewe, isipokuwa ni kutoka kwa wale wenye kushikamana na ulinganizi wa haki – kusema wakati wanapokusanyika kwa ajili ya kula:

“Ee ndugu! Leta chumvi!”

Kwa nini? Ndio, wanataka kuanza chakula kwa chumvi. Kwa sababu Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Yule mwenye kuanza chakula chake kwa chumvi, basi anapata ponyo ya maradhi sabini.”

Hii ni Hadiyth iliyotungwa. Kwa nini wafanya hivo? Kwa sababu hawana elimu.

Wakati nilipokuwa al-Madiynah al-Munawwarah na miji mingine, niliulizwa maoni yangu kuhusu Jamaa´at-ut-Tabliygh. Nyinyi ni Jamaa´at-ut-Tabliygh. Mimi nawaambieni ukweli kabisa:

Jamaa´at-ut-Tabliygh ni Suufiyyah wa sasa! Suufiyyah wa leo!

Nini maana ya Suufiyyah? Ni mrengo. Alikuwepo Shaykh mmoja huko India ambaye amesoma kutoka kwa Qaadiriyyah, Naqshbandiyyah na kadhalika… mnalijua hili au hamlijui? Ni vipi mtu kama huyu atalingania katika Qur-aan na Sunnah atasema:

“Uokozi wetu na kufaulu kwetu duniani na Aakhirah ni kwa kufuata maamrisho ya Allaah na Sunanh za Mtume.”?

Sunnah iko wapi ilihali Mola wetu anasema:

وَلَا تَكُونُوا مِنَ الْمُشْرِكِينَ مِنَ الَّذِينَ فَرَّقُوا دِينَهُمْ وَكَانُوا شِيَعًا

“… na wala msiwe miongoni mwa washirikina; miongoni mwa wale walioifarikisha dini yao wakawa makundimakundi.”[1]

Sisi tunatosheka na madhehebu manne[2]. Hapana. Amekuja na mrengo wa nne. Mirengo arobaini. Mirengo hii yote haitoshi. Baadaye kumekuja mapote ya siasa, mapote yenye mwelekeo wa kijamii, mapote ya kiuchumi na kadhalika. Vipi mtu atazungumzia uokozi na mafanikio wakati kiongozi wa kundi hili anafanyia kazi mrengo mmoja baada ya mwingine. Naqshbandiyyah wanasema:

“Wakati mwanafunzi anapomtaja Allaah, basi hatakiwi kufikiria ukubwa wa Allaah. Bali anatakiwa kumfikiria mwalimu wake.”

Wanaona kuwa mwalimu ndiye anayemfikisha kwa Mola. Sisi huko Shaam tuko na mrengo wa Naqshbandiyyah. Wanaweka picha ya mwalimu mbele yao upande wa Qiblah. Wanaiangaza picha hiyo kwa mataaa mpaka picha hiyo iingie katika mawazo ya mwanafunzi huu. Afanye nini? Amtaje Allaah. Ni nani anayemchunga? Mwalimu. Mtu hawezi kumfikia Allaah pasi na mwalimu.

Kwa hivyo uokozi na mafanikio yetu ni katika kuisoma Sunnah na kuietea kazi.

[1] 30:31-32

[2] ´Allaamah at-Tuwayjiriy (Rahimahu Allaah) amesema:

“Tabliyghiyyuun ni wenye kushikamana na mirengo minne ya Suufiyyah; Jishtiyyah, Sahruurdiyyah, Qaadiriyyah na Naqshbandiyyah.” (al-Qawl al-Baliygh, uk. 11)

  • Mhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Silsilat-ul-Hudaa wan-Nuur (540)
  • Imechapishwa: 20/05/2022