Swali 51: Ni matukio gani yalitokea mwaka huo?

Jibu: Sa´d bin Mu´aadh alikufa baada ya kutoa hukumu ya kuuliwa kwa Banuu Quraydhwah.

Mwaka huohuo, baada ya Banuu Quraydhwah, aliuliwa Ibn Abiyl-Huqayq na watu watano kutoka katika kabila la Khazraj. Mtu ambaye alisimamia mauaji hayo alikuwa ni ´Abdullaah bin ´Atık. Kisha baada yake akauliwa Khaalid bin Nabiyh al-Hudhaliy na ́Abdullaah bin Unays.

Katika mwaka huohuo Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam) akamuoa Zaynab bint Jahsh na kabla ya hapo Umm Habiybah bint Abiy Sufyaan.

Katika mwaka huo kuliteremshwa Aayah nyingi kutoka katika Suurah ”al-Ahzaab”, kukiwemo Aayah inayohusu Hijaab.

  • Mhusika: ´Allaamah Haafidhw bin Ahmad al-Hakamiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Amaaliy fiys-Siyrah an-Nabawiyyah, uk. 114-115
  • Imechapishwa: 17/10/2023