Imaam an-Nawawiy (Rahimahu Allaah) amesema:

عن الزبير بن عدي، قَالَ: أتينا أنسَ بن مالك رضي الله عنه فشكونا إِلَيْه مَا نلقى مِنَ الحَجَّاجِ. فَقَالَ: (اصْبرُوا؛ فَإنَّهُ لا يَأتي عَلَيْكُم زَمَانٌ إلا والَّذِي بَعدَهُ شَرٌّ مِنهُ حَتَّى تَلقَوا رَبَّكُمْ) سَمِعتُهُ مِنْ نَبِيِّكُمْ صلى الله عليه وسلم. رواه البخاري

92 – az-Zubayr bin ´Adiyy (Radhiya Allaahu ‘anh) amesema: “Kuna watu walimjia Anas bin Maalik (Radhiya Allaahu ´anh) na kumshtakia yanayowasibu kutoka kwa al-Hajjaaj. Akawaambia: “Kuweni na subira. Kwani hakutokuja zama isipokuwa ilio baada yake ni yenye shari zaidi kuliko iliyokutwa [hali itaendelea kuwa hivo] mpaka mkutane na Mola Wenu.” Nimeyasikia hayo kutoka kwa Mtume wenu (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam).

Ameipokea al-Bukhaariy

Katika Hadiyth hii kuna faida ya kutahadhari na zama mbaya na kwamba zama zinabadilika. Zinabadilika kwenda katika zama ilio na shari zaidi [kuliko ya kabla yake]. Siku moja Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) aliwaambia Maswahabah zake:

“Yule atayeishi kipindi kirefu katika nyinyi basi ataona tofauti nyingi.”[1]

Nafikiri sisi tumeishi duniani kidogo ukilinganisha na wale waliotangulia. Hata hivyo tunaona makinzano na tumeona tofauti nyingi, kati ya miaka iliyopita na miaka ya sasa.

[1]Abu Dawuud (4607).

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Riyaadh-is-Swaalihiyn (02/38-39)
  • Imechapishwa: 17/10/2023