Swali 50: Je, imamu aweke mtu mwingine maeneo pake pale ambapo unachenguka wudhuu´ wake au zinaharibika swalah za wote au amwamrishe ambaye atawaswalisha upya?

Jibu: Maoni ya sawa ni kwamba kilichosuniwa ni imamu ateue ambaye atawakamilishia swalah yao. Hivo ndivo alivyofanya ´Umar (Radhiya Allaahu ´anh) wakati alipodungwa ndani ya swalah alimteua ´Abdur-Rahmaan bin ´Awf (Radhiya Allaahu ´anh) ambapo akawakamilishia swalah ya Fajr. Kama imamu hakuteua mtu basi atasogea mmoja katika wale walioko nyuma yake na atawakamilishia watu swalah yao. Hapana vibaya akianza kuwaswalisha mwanzo. Kwa sababu suala hili kuna makinzano kati ya wanazuoni. Lakini maoni yaliyo na nguvu zaidi ni kwamba imamu atateua ambaye atawakamilishia swalah yao kutokana na yale tuliyoyataja katika kitendo cha ´Umar (Radhiya Allaahu ´anh). Akianza mwanzo hakuna vibaya.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa Muhimmah, uk. 55-56
  • Imechapishwa: 05/09/2022