50. Ni ipi hukumu ya kumswalia mtu aliyekufa mbali?

Swali 50: Ni ipi hukumu ya kumswalia mtu aliyekufa mbali[1]?

Jibu: Kilichotangaa ni kwamba ni jambo maalum kwa an-Najaashiy. Wako wazuoni wengine ambao wamelijuzisha ikiwa aliyekufa ana umuhimu katika Uislamu au ni mwanachuoni ambaye ana uchangamfu katika kulingania kwa Allaah na kueneza elimu na amekufa mbali. Huyu wanaona kuwa ataswaliwa. Lakini hatujafikiwa na kwamba (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alimswalia mwengine asiyekuwa an-Najaashiy. Haikupokelewa kutoka katika njia yoyote Swahiyh ya kwamba (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alimswalia mbali na na-Najaashiy. Wapo Maswahabah wengi waliokuwa Makkah na kwenginepo na wala haikuthibiti kuwa (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) aliwaswalia.

Kwa kumalizia ni kwamba maoni ya waliosema kuwa ni jambo maalum kwake yana nguvu. Akifanya hivo pamoja ambao wana umuhimu katika Uislamu ambao wanafanana na an-Najaashiy miongoni mwa wanazuoni na watawala ambao wana umuhimu katika Uislamu, basi tunataraji kwamba hakuna vibaya katika kufanya hivo.

[1] Majmuu´-ul-Fataawaa (13/158).

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Ahkaam-ul-Janaa-iz, uk. 38-39
  • Imechapishwa: 24/12/2021