50. Matahadharisho ya Mtume (صَلَّى اللّٰهُ عَلَيْهِ وَسَلَّم) juu ya wapotevu na Ahl-ul-Bid´ah

Imepokelewa Hadiyth Swahiyh kutoka kwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ya kwamba amesema:

“Ukiwaona wale wanaofuata Aayah zisizokuwa wazi ndani yake [yaani Qur-aan], basi hao ndio wale ambao Allaah kawasema [katika Qur-aan]; hivyo tahadhari nao.”[1]

MAELEZO

Imesihi kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) katika Hadiyth iliyopokelewa na al-Bukhaariy na Muslim ya kwamba amesema:

“Ukiwaona wale wanaofuata Aayah zisizokuwa wazi ndani yake… “

Bi maana katika Qur-aan na Sunnah na wakawa wanachukua dalili za jumla na wanaacha dalili zilizopambanuliwa:

“… basi hao ndio wale ambao Allaah kawasema… “

Katika Aayah hii:

فَأَمَّا الَّذِينَ فِي قُلُوبِهِمْ زَيْغٌ فَيَتَّبِعُونَ مَا تَشَابَهَ مِنْهُ

“Ama wale ambao katika nyoyo zao mna upotovu, hufuata zile zisizokuwa wazi… “

“… hivyo tahadhari nao.”

Bi maana tahadharini na wale wenye mfumo huu ili wasikutatizeni dini yenu. Hapa kuna matahadharisho ya wanachuoni wapotevu na watu wa Bid´ah ili wasije kututatiza dini yetu. Hawa ni miongoni ya wale ambao:

يَنقُضُونَ عَهْدَ اللَّـهِ مِن بَعْدِ مِيثَاقِهِ وَيَقْطَعُونَ مَا أَمَرَ اللَّـهُ بِهِ أَن يُوصَلَ وَيُفْسِدُونَ فِي الْأَرْضِ

“Wanaovunja ahadi ya Allaah baada ya kwishaifunga na wanakata aliyoyaamrisha Allaah kuungwa na wanafanya ufisadi katika ardhi.” (02:27)

[1] al-Bukhaariy (4273), Muslim (2665), at-Tirmidhiy (2994), Abu Daawuud (4598), Ibn Maajah (47), Ahmad (06/48) na ad-Daarimiy (145).

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Kashf-ish-Shubuhaat, uk. 69
  • Imechapishwa: 30/12/2016