Miongoni mwa ajabau ya maajabu ni kuwa mja anaamini maisha ya milele lakini pamoja na hivyo anafanya bidii juu ya maisha ya udanganyifu. Pindi Allaah anapompenda mtu basi humkinga na dunia hii kama jinsi anavyowakinga wagonjwa wenu kutokamana na maji.

Ibn Abiyd-Dunyaa amepokea katika kitabu “Dhamm-ud-Dunyaa” ya kwamba Maalik bin Diynaar amesema:

“Kulisemwa kuambiwa ´Aliy (Radhiya Allaahu ´anh): “Ee Abu Hasan! Tueleze maisha ya dunia hii.” Akasema: “Kwa kirefu au kwa kifupi?” Wakasema: “Kwa kifupi.” Akasema: “Yale ya halali yake ndani yake mtu atayalipia hesabu na yale ya haramu yake ndani yake mtu ataadhibiwa kwa Moto.”

Yuunus bin ´Ubayd amesema:

“Dunia hii ni kama mwanaume aliyelala na akaota ndoto mbaya na ndoto nzuri. Tahamaki ghafla akaamka.”

al-Hasan bin ´Aliy amesema:

“Dunia ni kivuli chenye kuondoka.”

Abu Sulaymaan ad-Daaraaniy amesema:

“Ikiwa Aakhirah ndio iko ndani ya moyo basi inakuja dunia hii na kuanza kusongamana. Ikiwa dunia hii ndio iko moyoni Aakhirah haiji kusongamana. Kwa kuwa Aakhirah ni tukufu na dunia hii ni yenye kulaumiwa.”

al-Awzaa´iy ameeleza kuwa amemsikia Bilaal bin Sa´iyd akisema:

“Ninaapa kwa Allaah inatosha kuwa dhambi kwa Allaah (´Azza wa Jall) kuona Allaah anaipa nyongo dunia hii ilihali sisi ni wenye kuikimbilia. Wapaji nyongo wenu wanataka, wafanya bidii wenu wanafanya upungufu na wanachuoni wenu ni wajinga.”

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Muhammad al-Hanbaliy al-Manbajiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Tasliyatu Ahl-il-Maswaa-ib, uk. 243
  • Imechapishwa: 31/12/2016