Tumewaomba Jahmiyyah, wanaodai kwamba Allaah yuko kila mahali na hakuna maeneo ambapo anakosekana, tuelezeni kuhusu maneno ya Allaah (´Azza wa Jall):

فَلَمَّا تَجَلَّىٰ رَبُّهُ لِلْجَبَلِ جَعَلَهُ دَكًّا وَخَرَّ مُوسَىٰ صَعِقًا

”Mola wako alipojidhihirisha katika jabali akalifanya livurugike kuwa vumbi na Muusa akaanguka hali ya kuzimia.”[1]

Ni vipi atajionyesha kwa mlima ikiwa mambo ni kama mnavodai kwamba yuko ndani yake? Angelikuwa ndani yake kama mnavyodai basi angejionyesha kwao. Lakini Allaah (Jalla wa ´Alaa) yuko juu ya ´Arshi na alijidhihirisha kwa kitu ambacho Yeye hakuwa ndani yake. Vilevile mlima uliona kitu ambacho haukupatapo kukiona kabla ya hapo[2].

[1] 7:143

[2] Ibn ´Aqiyl al-Hanbaliy amesema:

”Imaam Ahmad (Rahimahu Allaah) ameandika kitabu kinachoitwa ”ar-Radd ´alaal-Jahmiyyah waz-Zanaadiqah wal-Qadariyyah.” (al-Aadaab ash-Shar´iyyah (1/274))

Ibn Taymiyyah amesema:

”Kama alivosema Imaam Ahmad katika kitabu chake ”ar-Radd ´alaaz-Zanaadiqah wal-Jahmiyyah.”  (Tafsiyr Suurat-il-Ikhlaasw, uk. 239)

Ibn Kathiyr amesema:

”… na hivo ndivo alivosema Ahmad bin Hanbal katika kitabu ”ar-Radd ´alaal-Jahmiyyah” (Tafsiyr al-Qur-aan al-´Adhwiym (3/304))

Ibn Hajar al-´Asqalaaniy amesema:

”Amesema waziwazi Ahmad katika kitabu “ar-Radd ´alaal-Jahmiyyah.” (Fath-ul-Baariy (13/598))

  • Mhusika: Imaam Ahmad bin Hanbal (afk. 241)
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: ar-Radd ´alaal-Jahmiyyah waz-Zanaadiqah, uk. 170-171
  • Imechapishwa: 05/05/2024