Kuhusu mbingu na ardhi vimekwishatoweka, kwa sababu wakazi wake ima wameingia Peponi au Motoni. Ama ´Arshi haitoteketea wala kuondoka, kwa sababu ndio paa la Peponi. Vilevile Allaah yuko juu yake, na kwa ajili hiyo kamwe haitoangamia wala kuteketea.

Kuhusu maneno Yake (Ta´ala):

وكُلُّ شَيْءٍ هَالِكٌ إِلَّا وَجْهَهُ

“Kila kitu ni chenye kuangamia isipokuwa uso Wake.”[1]

Ni pale ambapo Allaah alipoteremsha:

كُلُّ مَنْ عَلَيْهَا فَانٍ

”Kila aliyekuwa humo [mbinguni na ardhini] atatoweka.”[2]

ambapo Malaika wakajiuliza watu wamekwishakufa na wao wenyewe walikuwa wakitamani kubaki. Ndipo Allaah (´Azza wa Jall) akateremsha Aayah ambayo akakhabarisha kuhusu wakazi wa Peponi na wakazi wa Motoni kwamba watakufa, nayo ni:

وكُلُّ شَيْءٍ هَالِكٌ

“Kila kitu ni chenye kuangamia…”[3]

Bi maana kila chenye kuishi kitakufa.

إِلَّا وَجْهَهُ

“…  isipokuwa uso Wake.”

Yeye yuhai na hatokufa. Hapo ndipo na wao wakayakinisha kwamba watakufa[4].

[1] 28:88

[2] 55:26

[3] 28:88

[4] Ibn ´Aqiyl al-Hanbaliy amesema:

”Imaam Ahmad (Rahimahu Allaah) ameandika kitabu kinachoitwa ”ar-Radd ´alaal-Jahmiyyah waz-Zanaadiqah wal-Qadariyyah.” (al-Aadaab ash-Shar´iyyah (1/274))

Ibn Taymiyyah amesema:

”Kama alivosema Imaam Ahmad katika kitabu chake ”ar-Radd ´alaaz-Zanaadiqah wal-Jahmiyyah.”  (Tafsiyr Suurat-il-Ikhlaasw, uk. 239)

Ibn Kathiyr amesema:

”… na hivo ndivo alivosema Ahmad bin Hanbal katika kitabu ”ar-Radd ´alaal-Jahmiyyah” (Tafsiyr al-Qur-aan al-´Adhwiym (3/304))

Ibn Hajar al-´Asqalaaniy amesema:

”Amesema waziwazi Ahmad katika kitabu “ar-Radd ´alaal-Jahmiyyah.” (Fath-ul-Baariy (13/598))

  • Mhusika: Imaam Ahmad bin Hanbal (afk. 241)
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: ar-Radd ´alaal-Jahmiyyah waz-Zanaadiqah, uk. 170
  • Imechapishwa: 05/05/2024