Tukawauliza Jahmiyyah kama Allaah ni nuru. Wakajibu kwamba Yeye wote ni nuru. Tukasema kwamba Allaah (Ta´ala) amesema:

وَأَشْرَقَتِ الْأَرْضُ بِنُورِ رَبِّهَا

”Ardhi itang’ara kwa nuru ya Mola wake.”[1]

Allaah (´Azza wa Jall) ameeleza kwamba Yuko na nuru. Midhali mnadai kuwa Allaah yuko kila mahali na kwamba Yeye ni nuru, tunakuulizeni ni kwa nini basi asiangaze chumba chenye giza, ambacho Yeye yumo ndani yake. Kwani nyinyi mnadai kuwa Allaah yuko kila mahali. Linawezaje taa kuangaza nyumba nzima? Hapo ndipo ukabaini nuwongo wao juu ya Allaah (Ta´ala).

Allaah amrehemu ambaye anamfikiria Allaah, akajirejea kutokana na maneno yake yanayoenda kinyume na Qur-aan na Sunnah, akazungumza kwa mujibu wa maneno ya wanazuoni, nayo ni yale maneno ya Wahamiaji na Wanusuraji, na akaachana na dini ya shaytwaan na dini ya al-Jahm na wafuasi wake.

Himdi zote njema anastahiki Allaah, Mola wa walimwengu. Swalah na amani zimwendee bwana wetu Muhammad, kizazi chake, Maswahabah zake na wale wale watakaowafata mpaka siku ya Qiyaamah[2].

Mwisho

[1] 39:69

[2] Ibn ´Aqiyl al-Hanbaliy amesema:

”Imaam Ahmad (Rahimahu Allaah) ameandika kitabu kinachoitwa ”ar-Radd ´alaal-Jahmiyyah waz-Zanaadiqah wal-Qadariyyah.” (al-Aadaab ash-Shar´iyyah (1/274))

Ibn Taymiyyah amesema:

”Kama alivosema Imaam Ahmad katika kitabu chake ”ar-Radd ´alaaz-Zanaadiqah wal-Jahmiyyah.”  (Tafsiyr Suurat-il-Ikhlaasw, uk. 239)

Ibn Kathiyr amesema:

”… na hivo ndivo alivosema Ahmad bin Hanbal katika kitabu ”ar-Radd ´alaal-Jahmiyyah” (Tafsiyr al-Qur-aan al-´Adhwiym (3/304))

Ibn Hajar al-´Asqalaaniy amesema:

”Amesema waziwazi Ahmad katika kitabu “ar-Radd ´alaal-Jahmiyyah.” (Fath-ul-Baariy (13/598))

  • Mhusika: Imaam Ahmad bin Hanbal (afk. 241)
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: ar-Radd ´alaal-Jahmiyyah waz-Zanaadiqah, uk. 171-172
  • Imechapishwa: 05/05/2024