50. ´Aqiydah ya Maswahabah wote kuhusu ujuu wa Allaah

48- Tayari imekwishatangulia ya kwamba ´Adiy bin ´Umayrah al-Abdiy kwamba amesema:

“Nikakumbuka maneno ya bn Shahlaa na nikahajiri kwenda kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Ndipo nikamuona yeye na Maswahabah wake wanasujudu juu ya nyuso zao na wanasema kuwa Mola wao yuko juu ya mbingu, ambapo nikasilimu na kumfuata.”

 Hii ni khabari kutoka kwao wote wao.

49- Kadhalika kumekwishatangulia yule mtumwa mweusi aliyekuja kwa Maswahabah wa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na akawauliza:

“Mtu huyu ni nani?”Wakasema: “Ni Mtume wa Allaah aliyetumwa na Allaah.” Akasema: “Yule aliye mbinguni?” Wakajibu: “Ndio.”

50- Vivyo hivyo inahusiana na mapokezi mengine yote yenye maana kama hii. Hapana shaka kwamba walikuwa wakiyasadikisha na wakionelea kuwa ni Swahiyh. Wakati mmoja wao alipowauliza Allaah (Ta´ala) yuko wapi ambapo wakajibu:

“Yuko juu mbinguni.”

51- Vilevile tumetaja mashairi ya Hassaan bin Thaabit na ya ´Abbaas bin Mirdaas ambaye aliimba mbele ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

Ametakasika Mola wetu aliye juu ya ´Arshi

Nafasi ya Allaah iko juu na ni kubwa

52- Abu ´Umar bin ´Abdil-Barr amesema:

“Tumepokea kupitia njia nyingi ambazo ni Swahiyh ya kwamba usiku mmoja ´Abdullaah bin Rawaahah  alienda kwa kijakazi wake na kufanya naye jimaa. Mke wake akamuona ambapo akamtupilia mbali. `Abdullaah akakanusha tuhuma ambapo mwanamke yule akamwambia:

“Ikiwa wewe ni mkweli basi soma Qur-aan. Kwani hakika mwenye janaba hasomi Qur-aan.” Ndipo akasema:

Nashuhudia kwamba ahadi ya Allaah ni haki

Na kwamba Moto ni makazi ya makafiri

Na kwamba ´Arshi iko juu ya maji

Na kwamba juu ya ´Arshi yuko Mola wa walimwengu

inabebwa na Malaika watukufu

Na Malaika wa Mungu ni wenye kuleta upepo

Mke wangu ambaye alikuwa hakuhifadhi Qur-aan akasema: “Umesema kweli na macho yangu ndio yamesema uongo.”[1]

 53- ´Abdullaah bin ´Abdir-Rahmaan as-Sulamiy ametukhabarisha: Abul-Qaasim al-Husayniy ametuhadithia: ´Abdul-´Aziyz al-Kinaaniy ametuhadithia: ´Abdur-Rahmaan bin ´Uthmaan ametuhadithia: Ami yangu Muhammad bin al-Qaasim ametuhadithia: Abu Bakr Ahmad bin ´Aliy bin Sa´iyd ametuhadithia: Abu Bakr bin Abiy Shaybah ametuhadithia: Abu Usaamah ametuhadithia, kutoka kwa Naafiy´ ambaye amesema:

“´Abdullaah bin Rawaahah alikuwa na kijakazi. Alikuwa akimficha mke wake kama wanalala naye. Siku moja akalala naye ambapo mke wake akamtuhumu kama amelala naye. Alipokanusha hilo akamwambia: “Basi soma Qur-aan sasa!”Ndipo akasema:

Nashuhudia kwa idhini ya Allaah ya kwamba Muhammad

ni Mtume wa Yule ambaye yuko juu ya mbingu

Na kwamba baba yake na Yahyaa na Yahyaa mwenyewe

wana mayendo yenye kukubaliwa mbele ya Mola

Ndipo akasema: “Una bahati.”[2]

54- Mashairi ya Umayyah bin Abiys-Swalt ni yenye kujulikana:

Mtukuze Allaah, na hakika ni Mwenye kustahiki kutukuzwa

Mola wetu Yuko juu ya mbingu, jioni imefika

kwa jengo kubwa ambalo limetangulia viumbe

Ameumba Kursiy juu ya mbingu

chin yake wako Malaika wanaotazama juu

Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Shairi lake limeamini na moyo wake ukakufuru.”[3]

[1] al-Isti´aab pamoja na ”al-Iswaabah” (2/296) ya Ibn Hajar.

[2] Ibn Abiy Shaybah (8/697).

[3] adh-Dhahabiy amesema:

”Cheni ya wapokezi imekatika.” (al-´Uluww, uk. 50)

  • Mhusika: Imaam Muwaffaq-ud-Diyn bin Qudaamah al-Maqdisiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Ithbaatu Swifat-il-´Uluww, uk. 145-147
  • Imechapishwa: 01/07/2018