Shaykh-ul-Islaam na Imaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab (Rahimahu Allaah) amesema:

Nguzo za swalah ni kumi na nne:

1- Kusimama kwa mwenye kuweza.

2- Takbiyr ya kufungulia swalah.

3- Kusoma al-Faatihah.

4- Rukuu´.

5- Kuinuka kutoka katika Rukuu´.

6- Kusujudu juu ya viungo saba.

7- Kuinuka kutoka katika Sujuud.

8- Kukaa baina ya Sajdah mbili.

9- Utulivu katika nguzo zote.

10- Kupangilia.

11- Tashahhud ya mwisho.

12- Kukaa katika Tashahhud ya mwisho.

13- Kumswalia Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam).

14- Tasliym.

MAELEZO

Hapa mtunzi wa kitabu (Rahimahu Allaah) anabainisha nguzo za swalah. Ameingiza kumswalia Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kuwa ni moja katika nguzo za swalah. Nguzo hizo ni:

 1- Kusimama kwa mwenye kuweza.

2- Takbiyr ya kufungulia swalah.

3- Kusoma al-Faatihah.

4- Rukuu´.

5- Kuinuka kutoka katika Rukuu´.

6- Kusujudu juu ya viungo saba.

7- Kuinuka kutoka katika Sujuud.

8- Kukaa baina ya Sajdah mbili.

9- Utulivu katika nguzo zote.

10- Kupangilia.

11- Tashahhud ya mwisho.

12- Kukaa katika Tashahhud ya mwisho.

13- Kumswalia Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam).

14- Tasliym.

Nguzo ni kitu ambacho ni lazima kipatikane na hakianguki si kwa kukusudia wala kwa kusahau. Tofauti kati ya nguzo na mambo ya wajibu ni kwamba jambo la wajibu linaanguka kwa kusahau au kwa kutokujua. Kuhusu nguzo ni kitu ambacho hakianguki si kwa kusahau, kwa kutokujua wala kwa kukusudia. Hilo linafahamishwa na Hadiyth ya yule mtu aliyeswali vibaya na akafunzwa na Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Pindi aliposwali kimakosa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alimwambia:

”Unaposimama kwa ajili ya swalah, basi timiza vizuri wudhuu´ wako. Halafu elekea Qiblah na kusema ”Allaahu Akbar”. Halafu soma kile kitachokuwepesikia katika Qur-aan… ”[1]

Nguzo hizi kumi na nne zitatajwa huko mbeleni kwa maelezo.

[1] al-Bukhaariy (6251).

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: ash-Sharh al-Mumtaaz, uk. 96-98
  • Imechapishwa: 01/07/2018