49. Dalili ya sita kutoka kwa Mtume kwamba Allaah yuko juu ya viumbe

47 – Muhammad bin ´Abdil-Baaqiy´ ametukhabarisha: Hamd bin Ahmad al-Haddaad ametuhadithia: Abu Nu´aym ametuhadithia: Baba yangu na Muhammad bin Ahmad wametuhadithia: al-Hasan ametuhadithia: Muhammad bin Humayd ametuhadithia: Ya´quub ametuhadithia, kutoka kwa Ja´far, kutoka kwa Sa´iyd bin Jubayr ambaye amesema:

“Watu walipatwa na ukame kwa miaka tatu katika ufalme wa mmoja katika wafalme wa wana wa Israaiyl. Mfalme akasema: “Allaah atatuteremshia mvua au tutamuudhi.” Waliokuwa wametangamana naye wakamwambia: “Vipi utaweza kumuudhi au kumkasirisha ilihali Yeye yuko juu mbinguni na wewe uko ardhini?” Akasema: “Nitamuua walii Wake ardhini.” Ndipo Allaah atawateremshia mvua kutoka mbinguni.”

  • Mhusika: Imaam Muwaffaq-ud-Diyn bin Qudaamah al-Maqdisiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Ithbaatu Swifat-il-´Uluww, uk. 144
  • Imechapishwa: 01/07/2018