Shaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab (Rahimahu Allaah) amesema:

Ngazi ya pili: Ni Imani. Imegawanyika sehemu sabini na kitu[1].

MAELEZO

Hii ndio ngazi ya pili miongoni mwa ngazi za dini bada ya ngazi ya Uislamu. Imani ni kusadikisha na kukubali kwa moyo, kukubali kwa ulimi na matendo ya moyo na matendo ya viungo vya mwili. Kwa hivyo imani imekusanya mambo manne:

1 – Maneno ya moyo. Kukubali na kuamini huku kunaingia katika imani. Nayo ni yale maneno ya moyo.

2 – Maneno ya mdomo. Ni kule kuyatamka maneno hayo.

3 – Matendo ya moyo. Kama vile khofu, shauku na woga.

4 – Matendo ya viungo vya mwili. Kama mfano wa swalah, swawm, zakaah na hajj.

Kwa hiyo imani inajumuisha kuitakidi kwa moyo, kukubali kwa mdomo, matendo ya moyo na matendo ya viungo vya mwili. Yote hayo ni katika imani.

Imani, kama alivobainisha (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) katika Hadiyth, ni sabini na kitu.

(البضع) ni kuanzia tatu mpaka tisa. Kwa msemo mwingine ni kuanzia sabini na tatu mpaka sabini na tisa. Hadiyth ya Abu Hurayrah (Radhiya Allaahu ´anh) aliyoipokea al-Bukhaariy ndio imetoa faida ya idadi hiyo ambapo (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

”Imani ni tanzu sitini na kitu.”

Muslim pia amepokea:

”Imani ni tanzu sabini na kitu.”

[1] al-Bukhaariy (09) na Muslim (35).

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Thalaathat-il-Usuwl, uk. 76-77
  • Imechapishwa: 13/02/2023