Shaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab (Rahimahu Allaah) amesema:

Ya juu yake ni neno “hapana mwenye haki ya kuabudiwa isipokuwa Allaah” na ya chini yake ni kuondosha kitu chenye kudhuru katika njia. Hayaa ni sehemu katika imani[1].

Nguzo zake ni sita: Kumuamini Allaah, Malaika Wake, Vitabu Vyake, Mitume Yake, kuamini siku ya Mwisho na uamini Qadar; kheri na shari yake[2].

Dalili ya nguzo hizi sita ni Kauli Yake (Ta´ala):

لَّيْسَ الْبِرَّ أَن تُوَلُّوا وُجُوهَكُمْ قِبَلَ الْمَشْرِقِ وَالْمَغْرِبِ وَلَـٰكِنَّ الْبِرَّ مَنْ آمَنَ بِاللَّـهِ وَالْيَوْمِ الْآخِرِ وَالْمَلَائِكَةِ وَالْكِتَابِ وَالنَّبِيِّينَ

“Si wema pekee kuelekeza nyuso zenu upande wa mashariki na magharibi, lakini wema wa kweli kabisa ni mwenye kuamini Allaah na siku ya Mwisho na Malaika na Kitabu na Manabii.”[3]

Dalili ya Qadar ni Kauli Yake (Ta´ala):

إِنَّا كُلَّ شَيْءٍ خَلَقْنَاهُ بِقَدَرٍ

”Hakika kila kitu Sisi Tumekiumba kwa makadirio.”[4]

MAELEZO

Amebainisha (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) tanzu ya imani ya chini na ya juu kabisa. Ni tanzu zenye kutofautiana; baadhi zinakaribiana. Kwa mfano swalah ni tanzu, zakaah ni tanzu, swawm ni tanzu, hajj ni tanzu, kuwatendea wema wazazi wawili ni tanzu, kuwaunga jamaa ni tanzu, kuamrisha mema na kukataza maovu ni tanzu.

Hayaa ni tanzu katika imani. Kwa maana nyingine ni tanzu ya kimoyo miongoni mwa matendo ya moyo. Hayaa ni sifa ya kindani inayomvuta mwenye nayo kufanya yanayompamba na inamzuia kufanya mambo yanayomfanya kuonekana mbaya.

Ubainifu huu wa nguzo za imani umechukuliwa katika Hadiyth ya Jibriyl wakati alipomuuliza Mtume (Swallla Allaahu ´alayhimaa wa sallam) kuhusu imani ambapo akajibu:

”Kumuamini Allaah, Malaika Wake, Vitabu Vyake, Mitume Yake, kuamini siku ya Mwisho na uamini Qadar ya kheri na ya shari yake.”

Ni nguzo sita.

[1] Muslim (08).

[2] Muslim (08).

[3] 02:117

[4] 54:49

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Thalaathat-il-Usuwl, uk. 78-79
  • Imechapishwa: 13/02/2023