Shaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab (Rahimahu Allaah) amesema:

Dalili ya kushuhudia ya kwamba Muhammad ni Mtume wa Allaah, ni Kauli Yake (Ta´ala):

لَقَدْ جَاءَكُمْ رَسُولٌ مِّنْ أَنفُسِكُمْ عَزِيزٌ عَلَيْهِ مَا عَنِتُّمْ حَرِيصٌ عَلَيْكُم بِالْمُؤْمِنِينَ رَءُوفٌ رَّحِيمٌ

“Hakika amekujieni Mtume anayetokana na nyinyi wenyewe, ni magumu juu yake yanayokutaabisheni, anakuhangaikieni, mwenye huruma mno na mapenzi tele kwa waumini.”[1]

Kushuhudia ya kwamba Muhammad ni Mtume wa Allaah maana yake ni kumtii katika yale aliyoamrisha, kumsadikisha kwa yale aliyoeleza, kujiepusha yale aliyokataza na kuyakemea na asiabudiwe Allaah isipokuwa kwa yale Aliyoyawekea Shari´ah.

Dalili ya swalah na zakaah na tafsiri ya Tawhiyd, ni Kauli Yake (Ta´ala):

وَمَا أُمِرُوا إِلَّا لِيَعْبُدُوا اللَّـهَ مُخْلِصِينَ لَهُ الدِّينَ حُنَفَاءَ وَيُقِيمُوا الصَّلَاةَ وَيُؤْتُوا الزَّكَاةَ ۚ وَذَٰلِكَ دِينُ الْقَيِّمَةِ

“Hawakuamrishwa jengine isipokuwa wamuabudu Allaah pekee hali ya kumtakasia yeye dini, wenye kupondoka kwenye haki na kuiacha batili, na wasimamishe swalah na watoe zakah – na hiyo ndiyo dini iliyosimama imara.”[2]

Dalili ya swawm ni Kauli Yake (Ta´ala):

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا كُتِبَ عَلَيْكُمُ الصِّيَامُ كَمَا كُتِبَ عَلَى الَّذِينَ مِن قَبْلِكُمْ لَعَلَّكُمْ تَتَّقُونَ

“Enyi mlioamini! Mmefaradhishiwa swawm kama ilivyoandikwa kwa walio kabla yenu – ili mumche.”[3]

Dalili ya hajj ni Kauli Yake (Ta´ala):

وَلِلَّـهِ عَلَى النَّاسِ حِجُّ الْبَيْتِ مَنِ اسْتَطَاعَ إِلَيْهِ سَبِيلًا ۚ وَمَن كَفَرَ فَإِنَّ اللَّـهَ غَنِيٌّ عَنِ الْعَالَمِينَ

”Kwa ajili ya Allaah ni wajibu kwa watu watekeleze hajj katika Nyumba hiyo kwa mwenye uwezo wa kuiendea. Na atakayekanusha, basi hakika Allaah ni mkwasi kwa walimwengu.”[4]

MAELEZO

Maneno Yake (Ta´ala):

لَقَدْ جَاءَكُمْ رَسُولٌ مِّنْ أَنفُسِكُمْ عَزِيزٌ عَلَيْهِ مَا عَنِتُّمْ حَرِيصٌ عَلَيْكُم بِالْمُؤْمِنِينَ رَءُوفٌ رَّحِيمٌ

“Hakika amekujieni Mtume anayetokana na nyinyi wenyewe, ni magumu juu yake yanayokutaabisheni, anakuhangaikieni, mwenye huruma mno na mapenzi tele kwa waumini.”

Bi maana yanamtia uzito (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) yale yanatokutieni uzito. Bi maana anapupia juu ya kuongoka kwenu na anajitahidi muweze kunufaika duniani na Aakhirah. Ni mwenye huruma na mapenzi kwa waumini.

Mtunzi (Rahimahu Allaah) amefasiri kuwa maana yake ni kumtii katika yale aliyoamrisha, kumsadikisha katika yale aliyoeleza, kujiepusha yale aliyokataza na kuyakemea na asiabudiwe Allaah isipokuwa kwa yale aliyoyawekea Shari´ah. Kuhusu ambaye anadai kuwa eti anashuhudia kuwa Muhammad ni Mtume wa Allaah hata hivyo hasadikishi maelezo yake, hatii maamrisho yake na wala hajiepushi makatazo yake ni mwongo na wala hayamnufaishi maneno yake.

Yeye (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ndiye Nabii wa mwisho. Dalili ni maneno Yake (Ta´ala):

مَّا كَانَ مُحَمَّدٌ أَبَا أَحَدٍ مِّن رِّجَالِكُمْ وَلَـٰكِن رَّسُولَ اللَّـهِ وَخَاتَمَ النَّبِيِّينَ

“Hakuwa Muhammad baba wa yeyote miongoni mwa wanaume wenu, lakini ni Mtume wa Allaah na ni mwisho wa Manabii.”[5]

Maneno Yake (Ta´ala):

وَمَا أُمِرُوا إِلَّا لِيَعْبُدُوا اللَّـهَ مُخْلِصِينَ لَهُ الدِّينَ حُنَفَاءَ وَيُقِيمُوا الصَّلَاةَ وَيُؤْتُوا الزَّكَاةَ ۚ وَذَٰلِكَ دِينُ الْقَيِّمَةِ

“Hawakuamrishwa jengine isipokuwa wamuabudu Allaah pekee hali ya kumtakasia yeye dini, wenye kupondoka kwenye haki na kuiacha batili, na wasimamishe swalah na watoe zakah – na hiyo ndiyo dini iliyosimama imara.”

Hii ndio maana ya Tawhiyd; ´ibaadah pamoja na kumtakasia nia Allaah. Mja amtakasie ´ibaadah Allaah na hivyo awe mja wa Allaah na mpwekeshaji; mwenye kujiengua kutokana na shirki na kwenda katika Tawhiyd.

Maneno Yake (Ta´ala):

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا كُتِبَ عَلَيْكُمُ الصِّيَامُ كَمَا كُتِبَ عَلَى الَّذِينَ مِن قَبْلِكُمْ لَعَلَّكُمْ تَتَّقُونَ

“Enyi mlioamini! Mmefaradhishiwa swawm kama ilivyoandikwa kwa walio kabla yenu – ili mumche.”

Maana ya mmeandikiwa ni mmefaradhishiwa. Hii ni dalili ya kufaradhishwa kwa swawm.

Maneno Yake (Ta´ala):

وَلِلَّـهِ عَلَى النَّاسِ حِجُّ الْبَيْتِ مَنِ اسْتَطَاعَ إِلَيْهِ سَبِيلًا ۚ وَمَن كَفَرَ فَإِنَّ اللَّـهَ غَنِيٌّ عَنِ الْعَالَمِينَ

”Kwa ajili ya Allaah ni wajibu kwa watu watekeleze hajj katika Nyumba hiyo kwa mwenye uwezo wa kuiendea. Na atakayekanusha, basi hakika Allaah ni mkwasi kwa walimwengu.”

Yanaonyesha kuwa ni lazima. Maana yake ni kwamba Allaah amewawajibishia watu kuhiji Nyumba.

Hizi ni nguzo tano za Uislamu kwa dalili zake.

[1] Ahmad (36/623) (22291).

[2] 98:05

[3] 02:183

[4] 03:97

[5] 33:40

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Thalaathat-il-Usuwl, uk. 74-75
  • Imechapishwa: 13/02/2023