49. Dalili inayofahamisha uola wa Allaah na kustahiki Kwake kuabudiwa

Shaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab (Rahimahu Allaah) amesema:

Dalili ni Kauli Yake (Ta´ala):

وَمِنْ آيَاتِهِ اللَّيْلُ وَالنَّهَارُ وَالشَّمْسُ وَالْقَمَرُ ۚ لَا تَسْجُدُوا لِلشَّمْسِ وَلَا لِلْقَمَرِ وَاسْجُدُوا لِلَّـهِ الَّذِي خَلَقَهُنَّ إِن كُنتُمْ إِيَّاهُ تَعْبُدُونَ

”Na katika alama Zake ni usiku na mchana, jua na mwezi. Hivyo basi msisujudie jua na wala mwezi, bali msujudieni Allaah Ambaye Aliyeviumba – ikiwa Yeye Pekee ndiye mnamwabudu.”[1]

MAELEZO

Hii ni dalili juu ya uola na uungu Wake (Subhaanahu wa Ta´ala):

وَمِنْ آيَاتِهِ اللَّيْلُ وَالنَّهَارُ وَالشَّمْسُ وَالْقَمَرُ

”Na katika alama Zake ni usiku na mchana, jua na mwezi. Hivyo basi msisujudie jua na wala mwezi.”

Jua na mwezi – Mwezi ni nyota kubwa inayoungaza ulimwengu. Ni siraji yenye mwanga mkali na yenye nguvu, kama alivosema Allaah (Ta´ala).

Mwezi ni nuru inayoangaza usiku na inawaangazia watu njia.

Miongoni mwa faida zake pia ni kuutengeneza ulimwengu kwa miti yake, matunda yake na bahari zake. Endapo jua litajificha kutokamana na ulimwengu basi ulimwengu ungelidhurika na shughuli nyingi za watu zingeliharibika. Vivyo hivyo iwapo mwezi ungelijificha. Mwezi pia una manufaa juu ya matunda na miti pamoja na kujua hesabu. Amesema (Ta´ala):

وَالْقَمَرَ نُورًا وَقَدَّرَهُ مَنَازِلَ لِتَعْلَمُوا عَدَدَ السِّنِينَ وَالْحِسَابَ

“Mwezi kuwa ni nuru na akaukadiria vituo ili mjue idadi ya miaka na hesabu.”[2]

يَسْأَلُونَكَ عَنِ الْأَهِلَّةِ ۖ قُلْ هِيَ مَوَاقِيتُ لِلنَّاسِ وَالْحَجِّ

“Wanakuuliza kuhusu miandamo ya mwezi. Sema: ”Hivyo ni vipimo vya nyakati kwa watu na Hajj.”[3]

Kupitia mwezi watu wanapata kujua nyakati na muda wa deni na muda wa eda za wanawake na nyakati za ´ibaadah, swawm na hajj. Vyote hivi vinajulikana kupitia hesabu iliyojengeka juu ya nuru hizi mbili; jua na mwezi. Hesabu za kijua na hesabu za kimwezi ndani yake kuna manufaa ya viumbe wote.

Miongoni mwa viumbe Vyake ni mbingu saba. Amesema (Ta´ala):

اللَّـهُ الَّذِي خَلَقَ سَبْعَ سَمَاوَاتٍ وَمِنَ الْأَرْضِ مِثْلَهُنَّ يَتَنَزَّلُ الْأَمْرُ بَيْنَهُنَّ لِتَعْلَمُوا أَنَّ اللَّـهَ عَلَىٰ كُلِّ شَيْءٍ قَدِيرٌ وَأَنَّ اللَّـهَ قَدْ أَحَاطَ بِكُلِّ شَيْءٍ عِلْمًا

“Allaah ni Yule ambaye ameumba mbingu saba na katika ardhi mfano wa hizo, inateremka amri kati yao ili mjue kwamba Allaah juu ya kila jambo ni Muweza na kwamba Allaah amekizunguka kila kitu kwa ujuzi.”

الَّذِي خَلَقَ سَبْعَ سَمَاوَاتٍ طِبَاقًا

“Ambaye Ameumba mbingu saba matabaka.”[4]

Baadhi ziko juu ya zengine. Mbingu ilio karibu na wingu la dunia, kisha inayofuatia kwenda mpaka mbingu ya saba. Juu ya vyote hivo kuna ´Arshi ya ar-Rahmaan (Subhaanahu wa Ta´ala).

Ardhi pia ni saba. Amesema (Ta´ala):

وَمِنَ الْأَرْضِ مِثْلَهُنَّ

“… na katika ardhi mfano wa hizo… “

Ni tabaka saba pia. Kila tabaka katika tabaka hizi na ardhi saba ndani yake kuna wakazi. Ndani ya mbingu kuna nyota, sayari, jua na mwezi na ndani ya ardhi kuna viumbe katika wanyama kwa aina zake mbalimbali, milima, miti, madini na bahari. Hizi ni miongoni mwa alama za Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) za kilimwengu zinazoonekana na kushuhudiwa.

[1] 41:37

[2] 10:05

[3] 02:189

[4] 67:03

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Thalaathat-il-Usuwl, uk. 107-109
  • Imechapishwa: 17/12/2020