48. Mtu akiwaswalisha watoto wa kiume wawili awaweke nyuma yake au upande wake wa kuume?

Swali 48: Mtu akiwaswalisha watoto wa kiume wawili awaweke nyuma yake au upande wake wa kuume? Je, kubaleghe ni sharti ya kupanga safu na mtoto?

Jibu: Kilichowekwa katika Shari´ah katika hali hii ni kuwaweka nyuma yake kama watuwazima ambao ´ibaadah ni yenye kuwawajibikia wakiwa na miaka isiyopungua saba. Vivyo hivyo endapo atakuwa mtoto na mtumzima ambaye ´ibaadah ni yenye kumuwajibikia atawaweka nyuma yake. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) siku moja alimswalisha Anas na yatima mmoja na akawaweka nyuma yake wakati Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikuwa amemtembelea bibi yake Anas. Hali kadhalika wakati siku moja Anas alipanga safu pamoja na Jaabir, Jabbaar katika Answaar aliwaweka nyuma yake.

Lakini akiwa ni mtu mmoja atamweka upande wake wa kulia. Ni mamoja ni mtumzima au mtoto. Wakati Ibn ´Abbaas alipanga safu pamoja na Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) katika swalah ya usiku akaenda kukaa upande wa kushoto alimvuta upande wa kuliani mwake. Vivyo hivyo Anas (Radhiya Allaahu ´anh) aliswali na Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) katika baadhi ya swalah zake zilizopendekezwa ambapo akamweka upande wa kuliani mwake.

Kuhusu mwanamke mmoja na zaidi watakuwa nyuma ya mwanamme. Haijuzu kwake kukaa safu moja na imamu wala pamoja na wanamme. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) wakati alimswalisha Anas na yatima alimweka Umm Sulaym, ambaye ni mama yake Anas, nyuma yao.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa Muhimmah, uk. 54
  • Imechapishwa: 01/09/2022