48. Hekima ya nne ya swawm: Tajiri kutambua neema ya Allaah juu yake

Miongoni mwa hekima za swawm ni kwamba tajiri anapata kutambua neema ya Allaah juu yake juu ya utajiri kwa vile Allaah amemneemesha chakula, kinywaji na jimai, mambo ambayo amewanyima viumbe wengi. Hivyo anapata kumshukuru Allaah kwa neema hizi na anamshukuru kwa wepesi huu. Sambamba na hilo anapata kumkumbuka nduguye fakiri ambaye huenda wakati mwingine analala akiwa ni mwenye njaa na hivyo akamkirimu kwa kumpa swadaqah aweze kuficha aibu yake na kuziba njaa yake. Kwa ajili hiyo ndio maana Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikuwa ni mkarimu zaidi ya watu na alikuwa mkarimu zaidi katika Ramadhaan wakati anapokutana na Jibriyl ambapo akamfunza Qur-aan.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majaalis Shahr Ramadhwaan, uk. 65
  • Imechapishwa: 18/05/2020