49. Hekima ya tano ya swawm: Kulipa mazoezi tumbo

Miongoni mwa hekima za swawm ni kujizoweza kulidhibiti tumbo na nguvu ya kujizuia makali yake mpaka mtu anakuwa ni mwenye kuweza kuihukumu na kuiongoza katika yale yaliyo na kheri na uokozi wake. Kwani hakika nafsi ni yenye kuamrisha maovu kwa wingi isipokuwa ile iliyorehemewa na Mola.

Pindi mtu anapoiachia hivyo nafsi yake basi inamsaidia au inamwingiza katika maangamivu. Lakini akimiliki jambo lake na akaitawala basi huwezi kuiongoza katika ngazi na malengo ya juu zaidi.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majaalis Shahr Ramadhwaan, uk. 65
  • Imechapishwa: 18/05/2020