48. Hakuna haja ya njia mpya za kulingania

Taratibu zilizowekwa katika Shari´ah ni zenye kutosha kiasi cha kwamba hakuna haja ya mifumo iliyozuliwa. Kwa sababu hakuna njia yoyote inayonufaisha ulinganizi, isipokuwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) aliichukua na akawawekea Shari´ah njia hiyo Ummah wake.

Khutbah zilizowekwa katika Shari´ah, kukiwemoKhutbah za ijumaa na Khutbah za swalah ya ´iyd, ni miongoni mwa njia yenye manufaa zaidi katika kulingania kwa sababu imamu huzungumzia yale mambo yote ambayo Ummahunayahitajia katika ´ibaadah, miamala, tabia na mienendo.

Duara za kielimu zilizokuwa zikifanywa na Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), Maswahabah zake na waliowafuatia, zinatosha katika kuieneza elimu kwa anayetaka kujifunza.

Maswali ya fatwa na mtu kujitolea fatwa mwenyewe kunasimamisha mambo ya dini ya waislamu na mambo yanayohusu dunia yao na kuwaongoza katika njia ambayo Allaah (Ta´ala) amewawekea katika Shari´ah.

Kupambana jihaad katika njia ya Allaah (Ta´ala) kunadhamini kueneza Uislamu ulimwenguni kote.

Kwa hivyo njia zilizowekwa katika Shari´ah ni nyingi sana na zinakidhi mahitaji ya ulinganizi katika kila zama na mahali.

  • Mhusika: Shaykh ´Abdus-Salaam bin Barjas Aal ´Abdil-Kariym
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Hujaj al-Qawiyyah ´alaa anna Wasaa-il-ad-Da´wah Tawqiyfiyyah, uk. 68
  • Imechapishwa: 23/05/2023