47. Zuia mifumo yote ya ulinganizi iliyoingizwa ndani

Inapokuja katika kuthibitisha kwamba mfumo wa kulingania ni lazima uwe kwa mujibu wa Qur-aan na Sunnah, amesema Shaykh Bakr Abu Zayd (Rahimahu Allaah):

“Uhakika wa ulinganizi – bi maana lengo – unatakiwa uafikiane na Qur-aan na Sunnah na hakuna nafasi ya Ijtihaad za watu. Uhakika wa ulinganizi ni jambo la kihakika na lisilobadilika. Uhakika wa ulinganizi ni jambo la kihakika na halibadiliki kwa kubadilika nyakati, mahali na hali. Aidha vyombo vya kueneza ulinganizi vinatakiwa kuafikiana na mfumo wa kinabii. Imesihi kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Yeyote atakayezua katika amri yetu hii kile kisichokuwemokitarudishwa.”[1]

Imekuja katika upokezi mwingine:

“Yeyote atakayefanya katika amri yetu hii kisichoafikiana na amri yetu kitarudishwa.”[2][3]

Hii ni baadhi ya mifano kuonyesha namna ambavyo wanazuoni wanaona kuwa mfumo wa kulingania unatakiwa kuafikiana na Qur-aan na Sunnah. Pengine yakazisafisha nyoyo kutokamana na takataka za Bid´ah zilizofungamana na ulinganizi. Huenda vilevile zikamfanya yule ambaye ni mwadilifu, ambaye anataka kujengea dalili kwa ile misingi iliyowekwa katika Shari´ah, kuzuia mifumo yote iliyoingizwa ndani inayochafua ulinganizi wa Salafiyyah, pasi na kujali ukubwa wa manufaa yake na zinavyojenga.

[1] Muslim (1718).

[2] al-Bukhaariy (2697).

[3] Hukm-ul-Intimaa’, uk. 157

  • Mhusika: Shaykh ´Abdus-Salaam bin Barjas Aal ´Abdil-Kariym
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Hujaj al-Qawiyyah ´alaa anna Wasaa-il-ad-Da´wah Tawqiyfiyyah, uk. 66-67
  • Imechapishwa: 23/05/2023