46. Ulinganizi ni lazima uwe kwa mujibu wa mfumo wa Salaf

Shaykh Hamuud at-Tuwayjiriy amethibitisha msingi huohuo kwa njia nzuri kabisa katika kitabu chake ”Tahdhiyr-ul-´Aaqil”. Ijapo maneno yake hapa yanahusu maigizo yaliyozuliwa, walakini ni msingi wenye nguvu unaoraddi mambo yote yaliyozuliwa. Amesema (Rahimahu Allaah) akimraddi mtunzi wa kitabu ”Hukm-ut-Tamthiyl fiyd-Da´wah ilaa Allaah”:

“Miongoni mwa makosa ya mtunzi ni kuwa anasema katika ukurasa wa 13 eti maigizo ni miongoni mwa njia za ulinganizi na mafunzo yanayokubalika katika Shari´ah. Kosa hili kubwa linaweza kujibiwa kwa njia nyingi:

1 – Yaliyowekwa katika Shari´ah ni yale yaliyowekwa katika Shari´ah na Allaah na kupitia Mtume Wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Ndani ya Qur-aan na Sunnah hakuna yanayofahamisha uwekwaji wa Shari´ah wa maigizo. Kwa hivyo madai hayo ni batili.

2 – Ni jambo la khatari sana kudai kuwa maigizo ni kitu kimewekwa katika Shari´ah kwa sababu ni kumsemea uwongo Allaah na Mtume Wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), jambo ambalo ni dhuluma na haramu iliokuwa kubwa.

3 – Kudai kuwa maigizo yamewekwa katika Shari´ah kunapelekea kuingiza ndani ya dini ambayo Allaah amewakamilishia waja Wake na akawaridhia kuifuata, jambo ambalo maana yake ni kuzidisha ndani ya dini na Shari´ah mambo ambayo hayakuidhinishwa na Allaah. Kuna matishio makali na dalili zinazoonyesha kuwa kitendo hicho ni dhuluma, ikiwa ni pamoja na maneno Yake Allaah (Ta´ala):

أَمْ لَهُمْ شُرَكَاءُ شَرَعُوا لَهُم مِّنَ الدِّينِ مَا لَمْ يَأْذَن بِهِ اللَّـهُ

“Je, wanao washirika waliowaamuru dini yale ambayo Allaah hakuyatolea kwayo idhini?”[1]

4 – Kudai kuwa maigizo yamewekwa katika Shari´ah kunapelekea kumtukana Allaah na Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na Maswahabah zake ya kwamba walipuuza jambo ambalo limewekwa katika Shari´ah katika kuwalingania na kuwafunza watu. Kwa maana ya kwamba hawakuutendea kazi wala kuwaelekeza watu katika mfumo huo. Miongoni mwa mambo ya khatari kabisa ni kumtukana Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na Maswahabah zake (Radhiya Allaahu ´anhum).

ash-Shaatwibiy amepokea kuwa Ibn Habiyb amesimulia kutoka kwa Ibn Maajashuun ambaye amesimulia kuwa amemsikia Maalik akisema:

“Yeyote ambaye atazua katika Uislamu uzushi na akaona kuwa ni mzuri, basi atakuwa amedai kuwa Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amefanya khiyana kwenye Ujumbe. Kwani Allaah (Ta´ala) amesema:

الْيَوْمَ أَكْمَلْتُ لَكُمْ دِينَكُمْ

”Leo nimekukamilishieni dini yenu.”[2]

Katika kitabu hichohicho ash-Shaatwibiy ametaja tamko lisemalo:

“Yeyote atakayezua katika Ummah huu kitu ambacho hakikufanywa na watangu wao, basi atakuwa amedai kuwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alisaliti Ujumbe. Kwani Allaah (Ta´ala) amesema:

الْيَوْمَ أَكْمَلْتُ لَكُمْ دِينَكُمْ وَأَتْمَمْتُ عَلَيْكُمْ نِعْمَتِي وَرَضِيتُ لَكُمُ الْإِسْلَامَ دِينًا

”Leo nimekukamilishieni dini yenu na nimekutimizieni neema Yangu na nimekuridhieni kwenu Uislamu uwe ndio dini yenu.” [3][4]

Ikiwa Maalik amesema namna hii juu ya mtu ambaye amezua ndani ya Uislamu uzushi ambao anaona kuwa ni mzuri, angelisema nini juu ya mtu ambaye anaona uzushi wa maigizo – ambao umezuliwa mwishoni mwa Ummah huu – kwamba ni miongoni mwa mifumo ya ulinganizi na mafunzo yaliyowekwa katika Shari´ah? Hapana shaka yoyote kwamba huku ni kukurupuka na kuchupa mipaka ambako ni khatari zaidi kuliko uzushi ambao Imaam Maalik (Rahimahu Allaah) alikufanyia ukali. Kwa hivyo afikirie maneno yake ya khatari ambayo maana yake ni kumtukana Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Azingatie maneno ya Imaam Maalik (Rahimahu Allaah), kwa sababu ni muhimu sana. Amche Allaah, atambue kuwa Shari´ah katika dini ni jambo la khatari mno na asijiaminishe pengine akawa mwenye kuingia ndani ya maneno Yake Allaah (Ta´ala):

أَمْ لَهُمْ شُرَكَاء شَرَعُوا لَهُم مِّنَ الدِّينِ مَا لَمْ يَأْذَن بِهِ اللَّهُ وَلَوْلَا كَلِمَةُ الْفَصْلِ لَقُضِيَ بَيْنَهُمْ وَإِنَّ الظَّالِمِينَ لَهُمْ عَذَابٌ أَلِيمٌ

”Leo nimekukamilishieni dini yenu na nimekutimizieni neema Yangu na nimekuridhieni kwenu Uislamu uwe ndio dini yenu. Lau si neno la uamuzi, bila shaka kungelihukumiwa kati yao. Hakika madhalimu watapata adhabu iumizayo.” [5]

Asijiaminishe pengine akawa mwenye kuingia ndani ya maneno Yake Allaah (Ta´ala):

لِيَحْمِلُوا أَوْزَارَهُمْ كَامِلَةً يَوْمَ الْقِيَامَةِ ۙ وَمِنْ أَوْزَارِ الَّذِينَ يُضِلُّونَهُم بِغَيْرِ عِلْمٍ ۗ أَلَا سَاءَ مَا يَزِرُونَ

 “Ili wabebe mizigo [ya madhambi] yao kamili Siku ya Qiyaamah na mizigo ya wale waliowapoteza bila ya elimu – Zindukeni! Uovu ulioje wanayoyabeba!”[6]

Asijiaminishe pengine akawa mwenye kuingia ndani ya maneno yake Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Na yeyote anayelingania katika upotofu basi anapata dhambi mfano wa dhambi za wataomfuata pasi na kupungua chochote katika dhambi zao.”[7]

Abu Hurayrah (Radhiya Allaahu ´anh) amesimulia kuwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Yeyote anayetoa fatwa pasi na elimu, basi dhambi zake zinarejea kwa yule aliyewatoleafatwa hiyo.”

Katika tamko lingine Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Yeyote anayetoa fatwa bila ya kuwa na uhakika, basi dhambi zake zinarejea kwa yule aliyewatoleafatwa hiyo.”[8]

Hivyo basi, yule muumini anayeitakia nafsi yake kheri atahadhari kuharakia kutoa fatwa pasi na elimu, kwa sababu ni jambo lenye matokeo mabaya kwa wanazuoni. Mwenye busara hatakiwi kuwa na jeuri juu ya kusema kuhusu kitu asichokuwa na elimu nacho kwamba hajui. Baadhi ya Salaf wamesema:

“Sijui ni nusu ya elimu.”

5 – Allaah (Ta´ala) amemwamrisha Mtume Wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kulingania katika njia Yake kwa hekima na maneno mazuri. Baadhi ya wafasiri wahakiki wamesema kuwa hekima ni Qur-ana na Sunnah na maneno mazuri ni yale makatazo na matukio yaliyowapata watu yaliyotajwa ndani ya Qur-aan. Huu ndio mwongozo wa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) katika kulingania na kufunza. Kuhusu maigizo yanayofanywa na baadhi ya watu hii leo na wanadai kuwa ni miongoni mwa mifumo ya kulingania na mafunzo yaliyowekwa katika Shari´ah sio katika mambo yaliyoamrishwa na Allaah katika Kitabu Chake. Wala sio katika mwongozo wa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) wala matendo ya Maswahabah, wanafunzi wa Maswahabah na wale waliowafuata kwa wema. Yule mwenye kwenda kinyume na mwongozo wa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na mfumo wa Maswahabah zake katika kulingania na kufunza basi kunakhofiwa juu yake kuingia ndani ya maneno Yake Allaah (Ta´ala):

وَمَن يُشَاقِقِ الرَّسُولَ مِن بَعْدِ مَا تَبَيَّنَ لَهُ الْهُدَىٰ وَيَتَّبِعْ غَيْرَ سَبِيلِ الْمُؤْمِنِينَ نُوَلِّهِ مَا تَوَلَّىٰ وَنُصْلِهِ جَهَنَّمَ ۖ وَسَاءَتْ مَصِيرًا

”Yule atakayempinga Mtume baada ya kuwa imeshambainikia uongofu na akaifuata njia isiyokuwa ya waumini, Tutamgeuza alikogeukia na tutamuingiza Motoni – na ni uovu ulioje mahali pa kuishia!”[9]

Kwa hivyo atahadhari yule muumini anayeitakia kheri nafsi yake asije kuingia ndani ya Aayah hii na huku akifikiri kuwa ameongozwa.”[10]

[1] 42:21

[2] 5:3

[3] 05:03 al-I´tiswaam.

[4] al-I´tiswaam.

[5] 02:21. Tazama “Naswaa’ih wa Fadhwaa’ih”, uk. 135-136, ya al-Waadi´iy.

[6] 16:25

[7]Ahmad, Abu Daawuud, an-Nasaa’iy, Ibn Maajah na at-Tirmidhiy aliyesema kuwa Hadiyth ni nzuri na Swahiyh. Ibn Hibbaan pia ameisahihisha. Cheni ya wapokezi wake ni Swahiyh. al-Haakim amepokea mfano wake na akasema kuwa ni Swahiyh juu ya sharti za al-Bukhaariy na Muslim. adh-Dhahabiy ameafikiana naye katika ”Talkhiysw-ul-Mustadrak”. 

[8] Ahmad, Ibn Maajah na ad-Daarimiy kwa cheni ya wapokezi nzuri.

[9] 4:115

[10] Tahdhiyr-ul-´Aaqil, uk. 19-23

  • Mhusika: Shaykh ´Abdus-Salaam bin Barjas Aal ´Abdil-Kariym
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Hujaj al-Qawiyyah ´alaa anna Wasaa-il-ad-Da´wah Tawqiyfiyyah, uk. 62-66
  • Imechapishwa: 23/05/2023