48. Hadiyth “Niombeeni kwa Allaah Njia… “

48 – Muhammad bin Abiy Bakr ametuhadithia: adh-Dhwahhaak bin Makhlad ametuhadithia: Muusa bin ´Ubaydah ametuhadithia: Muhammad bin ´Amr bin ´Atwaa’ amenikhabarisha, kutoka kwa Ibn ´Abbaas, kutoka kwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), ambaye amesema:

سلوا الله لي الوسيلة، لا يسألها لي مسلم أو مؤمن إلا كنت له شهيداً، أو شفيعاً، أو شفيعاً أو شهيداً

”Niombeeni kwa Allaah Njia (الوسيلة). Hakuna muislamu au muumini yeyote atakayeniombea nayo, isipokuwa nitamshuhudilia au kumfanyia uombezi, au kumfanyia uombezi au kumshuhudilia.”[1]

[1] Dhaifu kwa sababu ya Muusa bin ´Ubaydah. Hata hivyo maana ya Hadiyth ni Swahiyh. Imesihi kwa Hadiyth ya Ibn ´Amr inayokuja (50).  Ibn Abiy Shaybah pia ameipokea kupitia kwa Muusa bin ´Ubaydah.

  • Mhusika: Imaam Ismaa´iyl bin Ishaaq al-Maalikiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fadhwl-us-Swalaah ´alaan-Nabiy, uk. 50
  • Imechapishwa: 18/01/2024
  • taaliki: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy