47 – Muhammad bin Abiy Bakr ametuhaditihia: Mu´tamir ametuhaditihia, kutoka kwa Layth, kutoka kwa Ka´b, kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), ambaye amesema:

صلوا عليَّ فإن صلاتكم عليَّ زكاة لكم، وسلوا الله لي الوسيلة

”Niswalieni. Kwani hakika du´aa zenu kwangu ni utakaso kwenu. Na niombeeni kwa Allaah Njia (الوسيلة).” Ima walimuuliza au yeye mwenyewe ndiye aliwaeleza. Akasema: ”Ni ngazi ya juu zaidi Peponi. Hakuna atakayeipata isipokuwa mtu mmoja, na nataraji mimi ndiye.”[1]

[1] Kuna Swahabah anayekosekana katika cheni ya wapokezi kwa sababu ya al-Layth. Kuna wengine mbali na Mu´tamir wameipokea kutoka kwake hali ya kuungana cheni ya wapokezi, kama ilivyobainishwa katika Hadiyth ilio kabla yake.

  • Mhusika: Imaam Ismaa´iyl bin Ishaaq al-Maalikiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fadhwl-us-Swalaah ´alaan-Nabiy, uk. 49-50
  • Imechapishwa: 18/01/2024
  • taaliki: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy